Hizbullah: Hatutaki mazungumzo na Israel, hatutaki makubaliano nao
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i132884-hizbullah_hatutaki_mazungumzo_na_israel_hatutaki_makubaliano_nao
Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imeandika barua ya wazi kuhusu mitego iliyowekwa na Wazayuni kupitia kile kinachodaiwa ni mazungumzo ya amani na kusema kuwa, lengo la mazungumzo hayo ni kulitwisha taifa la Lebanon siasa za upande mmoja za Israel na kuvunja nguvu mwamko wa wananchi wa Lebanon wa kupigania haki zao mbele ya adui mpenda vita. Imesema: Mapambano ndiyo yanayolifanya taifa kubaki kuwa na heshima.
(last modified 2026-02-05T09:20:29+00:00 )
Nov 06, 2025 23:06 UTC
  • Hizbullah: Hatutaki mazungumzo na Israel, hatutaki makubaliano nao
    Hizbullah: Hatutaki mazungumzo na Israel, hatutaki makubaliano nao

Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imeandika barua ya wazi kuhusu mitego iliyowekwa na Wazayuni kupitia kile kinachodaiwa ni mazungumzo ya amani na kusema kuwa, lengo la mazungumzo hayo ni kulitwisha taifa la Lebanon siasa za upande mmoja za Israel na kuvunja nguvu mwamko wa wananchi wa Lebanon wa kupigania haki zao mbele ya adui mpenda vita. Imesema: Mapambano ndiyo yanayolifanya taifa kubaki kuwa na heshima.

Katika taarifa yake rasmi kupitia barua hiyo ya wazi kwa Rais, Waziri Mkuu, Spika wa Bunge na wananchi wa Lebanon, Hizbullah ilisema jana Alkhamisi kwamba, inaendelea kuheshimu kikamilifu masharti ya kusitisha mapigano tangu wakati yalipowekwa hadi leo hiii.

Taarifa hiyo imesema kwamba, utawala wa Kizayuni unaendelea kukanyaga makubaliano ya kusitisha mapigano kwa kufanya mashambulizi ya ardhini, baharini na angani, na hakuna ishara zozote kwamba uadui huo wa Israel kuna siku utasimama.

Hizbullah imekosoa pia uamuzi wa pupa uliochukuliwa na serikali ya Lebanon ambao umeonesha udhaifu wa serikali hiyo mbele ya mashinikizo ya Wazayuni na kusema kwamba, baadhi wanajaribu kuhalalisha uamuzi huo kwa kudai kuwa ni kuonesha "nia njema" kwa adui na wafuasi wake wakishindwa kutambua kwamba hatua hiyo imefungua njia kwa adui kushinikiza zaidi na kufikia hata kujipa uthubutu wa kutaka Muqawama wa Lebanon upokonywe silaha.

Harakati hiyo ya Muqawama wa Kiislamau ya Lebanon imeonya pia kwamba Israel haiilengi Hizbullah tu, bali inailenga Lebanon na watu wake wote. Hivyo, kupambana na njama za Israel kunahitaji kuwa na msimamo imara wa kitaifa, umoja na kulinda heshima ya taifa sambamba na kulindwa umoja wa ardhi yote ya Lebanon. 

Imesema, Israel ndiye adui nambari moja ambaye anasaidiwa na dhalimu mwenzake Marekani na ndio maana Hizbullah inasisitiza kuwa, adui kama huyo huwezi kupambana naye kwa michezo ya kisiasa na kulegeza misimamo mbele yake.