-
Je, Umoja wa Mataifa na jamii ya kimataifa zina nafasi gani katika kukabiliana na uchokozi wa Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran?
Jul 01, 2025 01:25Katika barua yake kwa Katibu Mkuu na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Seyyed Abbas Araqchi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza juu ya kuwajibishwa kisheria utawala wa Kizayuni na Marekani kufuatia hatua zao za kichokozi dhidi ya Iran.
-
Iran yataka Umoja wa Mataifa ulaani uchokozi wa Marekani na Israel
Jul 01, 2025 01:02Katika barua rasmi iliyowasilishwa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Rais wa Baraza la Usalama, Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa, Balozi Amir Saeid Iravani, siku ya Jumatatu ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kutambua Israel na Marekani kama wavamizi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Rais Pezeshkian: Mienendo ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki inaibua wasiwasi
Jun 30, 2025 23:04Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: "Mienendo ya hivi karibuni ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) inatia wasiwasi na inasababiisha changamoto kubwa kwa imani ya umma ya taifa la Iran."
-
Iran yasema inafuatilia kwa karibu harakati zozote za Israel katika nchi jirani
Jun 30, 2025 07:46Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza kuwa inafuatilia kwa karibu hatua zozote za utawala wa Kizayuni wa Israel zinazolenga kutumia ardhi ya nchi jirani kwa ajili ya vitendo vya uchokozi dhidi yake.
-
Araghchi: Iran ni muathiriwa mkuu wa silaha za kemikali hivyo inazipinga
Jun 30, 2025 07:38Abbas Araghchi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kama taifa lililoathirika zaidi na silaha za kemikali katika historia ya sasa, ni mtetezi imara wa dunia isiyo na silaha za maangamizi.
-
Larijani: Israel ilipanga lakini ilishindwa kumuua Kiongozi Muadhamu wa Iran
Jun 30, 2025 07:32Mshauri wa ngazi ya juu wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyyed Ali Khamenei, amefichua kuwa Israel ilikuwa imepanga kushambulia mkutano wa ngazi ya juu wa maafisa wa Iran—wakiwemo viongozi wa serikali—na baadaye kumlenga Kiongozi Muadhamu mwenyewe, lakini mpango huo ulizimwa kwa mafanikio.
-
Iravani: Hakuna mazungumzo na Marekani iwapo nchi hiyo inataka kuitwisha Iran sera zake
Jun 30, 2025 04:29Saeid Iravani Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa mazungumzo yoyote hayatawezekana na Marekani chini ya mashinikizo na kwa kuilaizmisha Iran sera zake.
-
Iran yalitaka Baraza la Usalama la UN kuzitambua Israel na Marekani kama pande zilizoanzisha uchokozi
Jun 30, 2025 04:16Abbas Araqchi Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liutambue utawala wa Israel na Marekani kuwa pande zilizoanzisha vita vya karibuni vya siku 12 dhidi ya Jamburi ya Kiislamu ya Iran.
-
Maulamaa Wakuu wa Iran: Shambulio lolote dhidi ya Kiongozi Muadhamu ni jinai ya kivita
Jun 30, 2025 02:29Maulamaa wakuu wa Kiislamu nchini Iran wamesema kuwa shambulio lolote au tishio dhidi ya Kiongozi Muadhamu na Marjai ni sawa na kutenda jinai ya kivita.
-
Je, Iran imekabiliana vipi na bwabwaja za Trump dhidi ya Kiongozi wa Mapinduzi?
Jun 30, 2025 02:16Bwabwaja na hambarara za Rais Donald Trump wa Marekani kuhusu Imam Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran zimekabiliwa na radiamali kali kutoka kwa viongozi wa Iran.