-
Ghalibaf: Hizbullah ipo hai na inaendelea na harakati zake
Oct 04, 2025 03:50Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran), Mohammad Bagher Ghalibaf amesisitiza kuwa Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon ingali "hai na inafanya kazi zake kama kawaida", huku ikiungwa mkono na wananchi wa nchi hiyo ya Kiarabu.
-
Iran yawanyonga magaidi wenye mfungamano na Israel
Oct 04, 2025 02:14Magaidi sita wanaohusishwa na utawala wa Kizayuni wa Israel wamenyongwa nchini Iran mapema leo Jumamosi.
-
Ayatullah Khatami: Njia ya kukabiliana na uvamizi na jinai ni muqawama na kusimama kidete
Oct 03, 2025 09:13Khatibu wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran amesema: "Njia ya kukabiliana na uvamizi na jinai za Wazayuni ni muqawama na kusimama kidete; njia hii imeonyesha kuwa njia pekee ya kuepusha dhulma ni kusimama kidete na kukabiliana na adui."
-
Rais Pezeshkian atoa wito wa umoja kwa ajili ya kukabili vitisho na vikwazo
Oct 03, 2025 04:30Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, ametoa wito wa mshikamano wa kitaifa na kutegemea imani pamoja na nguvu ya wananchi katika kukabiliana na vitisho na vikwazo, akisisitiza kuwa mauaji ya kisiasa, mashinikizo ya kijeshi na ukandamizaji wa kiuchumi haviwezi kulifanya taifa lake kusalimu amri.
-
Iran yapongeza utekelezaji wa Mkataba wa Ushirikiano wa Kistratejia na Russia
Oct 03, 2025 04:24Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imepongeza kuanza kutekelezwa kwa mkataba mpana wa ushirikiano wa kistratejia kati ya Iran na Russia.
-
Wananchi wa Iran waadhimisha kumbukizi ya kuuawa shahidi Nasrullah
Oct 03, 2025 00:01Wananchi Waislamu wa Iran wamefanya marasimu ya kumbukumbu ya mwaka mmoja ya kuuawa shahidi Sayyid Hassan Nasrullah, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon.
-
IRGC yasema iko tayari kujibu uchokozi wowote wa adui kwa nguvu zaidi
Oct 03, 2025 00:00Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limeonya kwamba, kitendo chochote kipya cha uadui dhidi ya Iran kitakabiliwa na jibu kubwa zaidi.
-
Dkt. Larijani: Marekani haina nia ya kufanya mazungumzo ya dhati
Oct 02, 2025 08:41Katibu wa Baraza Kuu la Usalama la Taifa la Iran amesema kuwa, Marekani haina nia ya dhati ya kufanya mazungumzo.
-
Iran: Uchokozi wa Israel dhidi ya msafara wa Sumud ni ugaidi na ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa
Oct 02, 2025 04:26Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imelaani vikali kitendo cha utawala ghasibu wa Israel cha kuivamia kijeshi msafara wa kimataifa wa meli unaojulikana kama Sumud uliokuwa ukielekea Ukanda wa Ghaza kwa ajili ya kufikisha misaada ya kibinadamu na kuvunja mzingiro Tel Aviv dhidi ya Ukanda wa Gaza.
-
Iran na Japan zafungua ukurasa mpya katika ushirikiano wa kisayansi
Oct 02, 2025 04:25Waziri wa Sayansi, Utafiti na Teknolojia wa Iran Hossein Simaee amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Japan nchini Iran Tamaki Tsukada kabla ya kufanya ziara huko Japan kwa lengo la kushiriki katika kikao cha 22 cha Kongamano la Sayansi na Teknolojia katika Jamii (STS).