-
Timu ya madaktari ya Iran yawasili Lebanon kusaidia wahanga wa hujuma ya kigaidi ya Israel
Sep 18, 2024 08:33Timu ya misaada ya kimatibabu ya Jumuiya ya Hilali Nyekundu ya Iran (IRCS) imewasili Lebanon kusaidia wahanga wa shambulio baya la kigaidi la utawala wa Israel katika nchi hiyo ya Kiarabu.
-
Qalibaf: Ugaidi ni sehemu ya hulka ya kutenda maovu ya utawala wa Kizayuni wa Israel
Sep 18, 2024 08:17Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amekutaja kuuwa watu wasio na hatia kuwa ni sehemu isiyotenganishika ya tabia na hulka ya kutenda maovu ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Rais Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran: Hatupendi vita, tunatetea haki zetu
Sep 18, 2024 02:43Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, Iran haijawahi kuwa, na wala haitakuwa mwanzishaji vita vyovyote vile na akabainisha kwamba: "wiki ijayo tutatetea haki za wananchi wa Iran katika Umoja wa Mataifa".
-
Araghchi: Kuunga mkono muqawama dhidi ya Israel ni 'sera ya kimsingi' ya Iran
Sep 18, 2024 01:10Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Sayyid Abbas Araghchi amesisitiza kuhusu sera thabiti ya Jamhuri ya Kiislamu ya kuunga mkono vikosi vya muqawama katika mapambano yao dhidi ya utawala ghasibu wa Israel.
-
Tehran, Beirut zajadili jinai mpya ya kigaidi ya Israel huko Lebanon
Sep 17, 2024 23:21Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi amelaani vikali hujuma mpya ya kigaidi ya utawala wa Kizayuni iliyowalenga raia wasio na hatia nchini Lebanon.
-
Iran: Israel lazima iwajibishwe kwa jinai ya kigaidi iliyofanya Lebanon
Sep 18, 2024 03:28Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amelaani ugaidi wa kimtandao uliofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel nchini Lebanon na kusema: Utawala wa Kizayuni lazima uwajibishwe kwa uchokozi na jinai hiyo ya kutisha.
-
Sisitizo la Kiongozi Muadhamu la ulazima wa umoja wa Umma wa Kiislamu
Sep 17, 2024 09:47Kwa miaka mingi, umoja wa ulimwengu wa Kiislamu ni miongoni mwa masuala makuu na ya kimsingi ambayo Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi amekuwa akiyasisitizia kila mara katika miongozo na jumbe zake kwa kuwapa nasaha wanachuoni, wasomi, viongozi wa kisiasa na Umma wa Kiislamu juu ya ulazima wa kuunda umoja wa jamii na serikali za Kiislamu.
-
Kiongozi Muadhamu: Sera za kindumakuwili za Magharibi zimedhihirika katika Michezo ya Olimpiki na Paralimpiki ya Paris
Sep 17, 2024 09:30Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Ali Khamanei, ameeleza kuchuuzwa kwake na sera za kinafiki na kindumakuwili zinazotumiwa na nchi zinazosimamia mashirikisho ya kimataifa ya michezo na kusema kuwa, sera hizo mbovu zilidhihirika wazi wakati wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya joto ya 2024 na Michezo ya Olimpiki ya Walemavu iliyomalizika hivi karibuni katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris.
-
Araghchi: Iran haijaipa Yemen makombora
Sep 17, 2024 04:02Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amekanusha vikali madai yasiyo na msingi ya Wamagharibi kuwa eti Yemen imepokea makombora kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Rais Pezeshkian: Hakuna mjadala kuhusu ulazima wa kukabiliana na Israel
Sep 16, 2024 23:35Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran jana alifanya mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari tangu aliposhika hatamu za uongozi akimrithi Sayyid Ibrahim Raisi aliyaeaga dunia katika ajali ya helikopta mwezi Meio mwaka huu.