Russia wavutiwa sana na bidhaa za nguo na ngozi za Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i120592-russia_wavutiwa_sana_na_bidhaa_za_nguo_na_ngozi_za_iran
Naibu wa Mkuu wa Mkoa wa Tehran katika masuala ya uratibu wa kiuchumi wa ametangaza habari ya kutiwa saini hati ya maelewano ya ushirikiano kati ya Iran na Russia katika masuala ya nguo na ngozi, baada ya wananchi wa Russia kuvutiwa sana na bidhaa za Iran.
(last modified 2024-12-25T08:45:47+00:00 )
Dec 25, 2024 08:45 UTC
  • Russia wavutiwa sana na bidhaa za nguo na ngozi za Iran

Naibu wa Mkuu wa Mkoa wa Tehran katika masuala ya uratibu wa kiuchumi wa ametangaza habari ya kutiwa saini hati ya maelewano ya ushirikiano kati ya Iran na Russia katika masuala ya nguo na ngozi, baada ya wananchi wa Russia kuvutiwa sana na bidhaa za Iran.

Hashmatoleh Asgari alitangaza habari hiyo jana Jumanne na katika hafla ya kutiwa saini mkataba wa ushirikiano kati ya Iran na Russia na kuongeza kuwa, mkataba huo wa ushirikiano wa sekta ya nguo ni wa kiistratijia.

Kwa mujibu wa Pars Today, Asgari amesema kuwa uchunguzi uliofanyika kuhusu masoko ya nchi hizi mbili unaonesha kuwa zina uwezo mkubwa wa kuzalisha kwa pamoja, kutembeleana wajumbe wa biashara na kubadilishana uzoefu na maarifa sambamba na kuweko urahisishaji wa kusafirisha bidhaa kati ya nchi mbili. Wote huo ni uwanja wa ushirikiano uliozingatiwa katika mkataba wa pamoja wa Tehran na Moscoa. Amesema upande wa Russia umejitolea kuwa na vitengo vingi vya kurahisisha kumiminika bidhaa za Iran nchini humo.

Kwa upande wake, Andrey Raz Brodin, mkuu wa Umoja wa Wajasiriamali wa Sekta ya Nguo ambaye pia ni mkuu wa Kituo cha Nguo cha Bunge la Russia ameelezea kuridhishwa kwake na kutiwa saini mkataba huo wa ushirikiano wa pamoja katika sherehe hiyo. Amesema hadi hivi sasa wamekuwa na ushirikiano na nchi za Pakistan China na Uturuki na ana matumaini ushirikiano wa Russia na Iran utakuwa na matunda mazuri.