Araghchi: Syria itashuhudia mabadiko makubwa
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i120596-araghchi_syria_itashuhudia_mabadiko_makubwa
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, ni mapema mno kutabiri mustakabali wa Syria hasa kwa wale wanaodhani kuwa wameshinda.
(last modified 2024-12-25T12:17:18+00:00 )
Dec 25, 2024 12:17 UTC
  • Araghchi: Syria itashuhudia mabadiko makubwa

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, ni mapema mno kutabiri mustakabali wa Syria hasa kwa wale wanaodhani kuwa wameshinda.

Sayyid Abbas Araghchi amesema na kuongeza kuwa: "Ni mapema mno kuhukumu mustakbali wa Syria, kuna mambo mengi yanayoathiri mustakbali wa nchi hii."

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema: "Kwa maoni yangu, ni mapema mno kutabiri, kwetu sisi na kwa wengine wanaofikiri kwamba wamepata ushindi; bila ya shaka kutakuwa na mabadiliko mengi katika siku zijazo."

Wapinzani wenye silaha na magaidi nchini Syria tarehe 27 Novemba 2024 walianzisha operesheni kaskazini magharibi, magharibi na kusini magharibi mwa mji wa Halab (Aleppo), na hatimaye, baada ya siku kumi na moja, tarehe 8 Disemba walichukua udhibiti wa Damascus, mji mkuu wa Syria baada ya kuondoka nchini humo Rais Bashar al Assad aliyeelekea Russia na familia yake. 

Kwa mujibu wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon), takriban wanajeshi elfu mbili wa Marekani wako katika maeneo yenye utajiri wa mafuta nchini Syria wakiendelea kupora utajiri wa nchi hiyo ya Kiarabu.

Benjamin Netanyahu, waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni alitangaza kuwa Israel haiheshimu tena makubaliano yake na Syria ya mwaka mwaka 1974 katika eneo la Golan, na jeshi la utawala huo lilivamia na kuteka maeneo ya kusini mwa Syria na kuyakalia kwa mabavu.

Jeshi la Uturuki lililoingia katika ardhi ya Syria miaka minane iliyopita yaani tarehe 24 Disemba 2016, linaendelea kuyakalia kwa mabavu maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo ya Kiarabu.