-
Iravani: Kutochukua hatua UN kunahalalisha haki ya Iran ya kujibu mashambulizi
Jul 19, 2026 03:20Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa, Amir Saeid Iravani, ameliandikia barua Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Katibu Mkuu wa umoja huo kufuatia uchokozi wa Marekani dhidi ya Iran, kushambuliwa miundombinu na mauaji ya raia wa Iran.
-
Op. Nasr-2: IRGC yaharibu rada ya kijeshi ya Marekani huko Kuwait katika shambulio la kulipiza kisasi
Jul 18, 2026 11:13Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limeharibu kituo cha rada cha jeshi la Marekani katika Kituo cha Anga cha Ali Al Salem na kushambulia mkusanyiko wa wanajeshi wa nchi hiyo katika Kambi ya Arifjan huko Kuwait katika wimbi la 18 la Operesheni Nasr 2.
-
Kamanda wa IRGC aapa kuendeleza mashambulizi 'yenye ufanisi' zaidi hadi utulivu utakaporejea nchini Iran
Jul 18, 2026 03:32Mkuu wa Kikosi cha Anga cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (IRGC) ameapa kwamba Jamhuri ya Kiislamu itaendeleza mashambulizi yake ya kulipiza kisasi "yenye ufanisi" hadi utulivu utakaporejeshwa kote nchini.
-
Kulipiza kisasi damu ya Imam shahidi kutaendelea hadi kuondoka Marekani katika eneo hili na kuangamia utawala wa Kizayuni
Jul 17, 2026 12:07Khatibu wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran amesema kuwa, kulipiza kisasi damu ya Imam shahidi kutaendelea hadi kuondoka Marekani katika eneo hili na kuangamia utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Iran yaendeleza mashambulizi dhidi ya Kambi za Jeshi la Marekani kulipiza kisasi jinai
Jul 17, 2026 04:14Kufuatia hujuma za kikatili za jeshi la kigaidi la Marekani dhidi ya madaraja kadhaa katika maeneo ya kusini mwa Iran, operesheni kubwa na endelevu ya makombora na droni za Iran imetekelezwa usiku wa kuamkia leo dhidi ya kambi za kijeshi za Marekani katika eneo la Asia Magharibi.
-
Jeshi la Iran: Udhibiti wa kimkakati wa Lango-Bahari la Hormuz sasa ni matakwa ya kitaifa
Jul 17, 2026 02:59Msemaji wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa suala la udhibiti wa kimkakati wa Mlango-Bahari wa Hormuz sasa limegeuka kuwa matakwa ya kitaifa, akisisitiza kuwa wananchi wa Iran wanaunga mkono hatua zinazolenga kulinda maslahi na usalama wa taifa katika njia hiyo muhimu ya kimataifa ya usafirishaji wa mafuta.
-
Iran yaonya italenga miundombinu yote ya eneo iwapo miundombinu yake itashambuliwa
Jul 16, 2026 10:51Iran imeonya kwamba italenga kila miundombinu iliyosalia katika eneo hili iwapo miundombinu yake itashambuliwa.
-
Qalibaf: Hakuna sababu ya kuendelea kuzingatia makubaliano na Marekani iwapo Iran hainufaiki
Jul 16, 2026 10:47Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Baqer Qalibaf, ameonya kwamba ikiwa Jamhuri ya Kiislamu haitanufaika na Mkataba wa Maelewano (MoU) wa Islamabad uliotiwa saini baina yake na na Marekani, basi hakuna sababu yoyote ya kuendelea kuufuata.
-
Iran yakemea shambulio la Marekani karibu na hospitali ya watoto huko Ahvaz
Jul 16, 2026 10:42Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekemea shambulio la Marekani karibu na hospitali ya watoto wanaougua saratani katika mji wa Ahvaz, kusini-magharibi mwa nchi, na kulitaja kuwa ni “uhalifu wa kivita wa kijinga na wa woga.” Taarifa zinasema shambulio hilo lililazimisha uokoaji wa dharura wa mamia ya wagonjwa walio katika hali hatarishi na pia limewatia hofu watoto wanaopatiwa matibabu ya saratani.
-
Mzunguko hatari wa vitisho vya Trump dhidi ya Iran
Jul 16, 2026 09:45Baada ya kushindwa kikamilifu mbinu zake zote za vikwazo, vitisho vya kijeshi na mashinikizo ya kisiasa, vitisho vipya vya Trump dhidi ya Iran vinaashiria wazi kushindwa kwake kimkakati, kabla ya kuwa ni dhihirisho la nguvu za Marekani.