-
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu atembelea maonyesho ya uwezo wa uzalishaji wa ndani
Jan 29, 2024 10:00Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, ametembelea maonyesho ya uwezo wa uzalishaji wa ndani ya Iran ambayo yamefanyika katika Hosseinieh ya Imam Khomeini (MA) leo asubuhi (Jumatatu).
-
Iran yasema haina uhusiano wowote na mashambulizi dhidi ya Marekani katika eneo la Asia Magharibi
Jan 29, 2024 09:32Ujumbe wa Iran katika Umoja wa Mataifa unasema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haina uhusiano wowote na mashambulizi dhidi ya vikosi vya Marekani katika eneo la Asia Magharibi na kwamba mashambulizi hayo yanahusiana na mzozo kati ya makundi ya muqawama (mapambano ya Kiisalmu) na jeshi la Marekani.
-
Iran yawanyonga magaidi wanne maajenti wa Mossad
Jan 29, 2024 09:16Idara ya Mahakama ya Iran imewanyonga watu wanne waliopatikana na hatia ya kufanya kazi na shirika la ujasusi la utawala haramu wa Israel, Mossad, na kupanga njama ya shambulio la bomu dhidi ya kiwanda cha Wizara ya Ulinzi katika mkoa wa Isfahan katikati mwa Iran.
-
Amir-Abdollahian: Mafanikio ya vijana wasomi wa Iran yanaonesha uwezo mkubwa wa ushirikiano na nchi rafiki
Jan 29, 2024 03:00Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameyataja mafanikio makubwa ya vijana wasomi wa nchi hii kuwa ni uthibitisho wa kuweko uwezo mkubwa wa kuendeleza diplomasia ya sayansi na ushirikiano katika uwanja wa teknolojia na nchi rafiki.
-
Iran yatuma angani satalaiti tatu kwa mafanikio
Jan 28, 2024 10:01Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imefanikiwa kutuma angani satalaiti tatu kwa mpigo zilizotengenezwa na wataalamu wa hapa nchini.
-
Kan'ani: Mashirika ya 'haki za binadamu' ya Magharibi hayana tena itibari
Jan 28, 2024 09:54Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema mashirika yanayojidai kuwa ya kutetea haki za binadamu katika nchi za Magharibi yamepoteza itibari na uhalali wao kwa kufumbia macho jinai za kutisha zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza.
-
Tehran: Iran na Pakistan hazitaruhusu maadui waharibu uhusiano wao wa kindugu
Jan 28, 2024 04:24Kufuatia shambulio lililowalenga raia wa Pakistan ndani ya Iran, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema Tehran na Islamabad hazitavumilia chokochoko za kuharibu uhusiano wa nchi hizo mbili.
-
Kukuza uhusiano na nchi za Afrika, moja ya mihimili ya sera za kigeni za Iran
Jan 28, 2024 01:05Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameutaja msingi wa uhusiano wa Tehran na nchi za Kiafrika kuwa ni mungamano wa kiroho baina ya mataifa hayo na kwamba uhusiano huo ni moja ya mihimili mikuu ya siasa za nje za Iran.
-
Kan'ani: Msingi wa Israel umejengwa kwa kutegemea mabavu na ubaguzi
Jan 27, 2024 08:55Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa jibu la kiuhasama lililotolewa na utawala wa Kizayuni wa Israel mkabala wa hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) linaonyesha namna msingi wa utawala huo ulivyojengwa kwa kutegemea vitendo vya mabavu na ubaguzi; na wakati huo huo unadhihirisha namna utawala huo usivyoheshimu kanuni na sheria za kimataifa.
-
Iran yaipongeza Afrika Kusini kwa ushindi wake katika mahakama ya ICJ dhidi ya Israel
Jan 27, 2024 03:01Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amepongeza mafanikio ya kidiplomasia ya Afrika Kusini katika Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu na kuwataka mawaziri wenzake wa mashauri ya kigeni duniani kuunga mkono hatua hiyo ya Afrika Kusini.