-
Raisi katika mazungumzo na Al-Sisi: Misri ifungue kivuko cha Rafah kwa ajili ya misaada kwa watu wa Gaza
Nov 12, 2023 09:00Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amemwambia mwenzake wa Misri, Abel Fattal Al Sisi kwamba, matarajio ya jumla ni kwamba kivuko cha Rafah kifunguliwe ili misaada ya kimataifa iweze kuingia Ukanda wa Gaza.
-
Rais Raisi: Utawala wa Kizayuni ndio chimbuko la masaibu mengi ya dunia yakiwemo ya Afrika
Nov 11, 2023 23:51Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekutana na kuzungumza na Mkuu wa Baraza la Utawala wa Sudan na kuutaja utawala wa Kizayuni kuwa balaa kubwa kwa Umma wa Kiislamu na ulimwengu mzima.
-
Iran na China zakubaliana kuanzisha kituo cha pamoja cha mafunzo ya teknolojia mpya
Nov 11, 2023 23:26Wakuu wa Idara za Mafunzo za Wizara za Sayansi, Utafiti na Teknolojia za Iran na China wamekubaliana juu ya kuanzishwa kituo cha pamoja cha utoaji mafunzo ya kiufundi na kitaalamu na mafunzo ya teknolojia mpya.
-
Rais Raisi: Vita vya Gaza ni makabiliano kati ya mhimili wa sharafu na mhimili wa uovu
Nov 11, 2023 11:28Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza katika kikao cha pamoja cha Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kwamba: kadhia ya Gaza ni makabiliano baina ya mhimili wa sharafu na mhimili wa uovu, na kila mtu anapaswa abainishe yuko upande gani.
-
Nukta tano muhimu katika barua ya Islami kwa Grossi kuhusiana na tishio la utawala wa Kizayuni kutumia bomu la nyuklia dhidi ya Ghaza
Nov 11, 2023 07:32Katika barua yake kwa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA, Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran amelitaka shirika hilo kulibainishia wazi Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, hatari zinazoweza kusababishwa na matumizi au tishio la matumizi ya silaha za nyuklia za utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi wa Palestina.
-
Mwakilishi wa Hamas nchini Iran alaani kimya cha nchi za Kiarabu dhidi ya jinai za utawala wa Kizayuni.
Nov 11, 2023 03:36Mwakilishi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas) nchini Iran amelaani kimya cha baadhi ya nchi za Kiislamu na Kiarabu mbele ya jinai za utawala wa Kizayuni.
-
Kikao cha ECO na sisitizo la kusimamishwa mashambulizi ya Israel Ukanda wa Ghaza
Nov 11, 2023 03:11Waziri Mkuu wa Pakistan, Anwaar-ul-Haq Kakar amesema katika kikao cha wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi (ECO) kilichofanyika Tashkent, mji mkuu wa Uzbekistan kwamba, tuna wajibu wa kuziunga mkono juhudi za kukomeshwa mashambilizi na jinai za kivita za utawala wa Kizyauni huko Ukanda wa Ghaza.
-
Kanani: Fedheha ya uungaji mkono wa Marekani kwa jinai za utawala wa Kizayuni haitafutika
Nov 11, 2023 01:14Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Nasser Kanani amesema: Marekani haitaweza kufuta fedheha kubwa ya uungaji mkono wake kwa utawala wa Kizayuni wa Israel ambao unawaua Wapalestina bila kujali.
-
Khatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran: Nchi za Kiarabu zinapaswa kukata uhusiano na utawala wa Kizayuni
Nov 10, 2023 08:07Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesisitiza ulazima wa serikali za nchi za Kiarabu kujibu ipasavyo matukio yanayojiri Ukanda wa Gaza na kusema: Jambo dogo kabisa linalotarajiwa kutoka kwa serikali za nchi za Kiarabu ni kukata uhusiano na utawala ghasibu wa Israel.
-
Kanani: Watoto wa Palestina daima wamekuwa ni jinamizi kwa Wazayuni
Nov 10, 2023 03:51Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa mjibizo kwa shambulio lililofanywa na utawala haramu wa Kizayuni dhidi ya Hospitali ya Watoto ya Al-Nasr huko Gaza, na kueleza kwamba: "watoto wa Kipalestina daima wamekuwa ni jinamizi kwa Wazayuni."