Kanani: Watoto wa Palestina daima wamekuwa ni jinamizi kwa Wazayuni
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa mjibizo kwa shambulio lililofanywa na utawala haramu wa Kizayuni dhidi ya Hospitali ya Watoto ya Al-Nasr huko Gaza, na kueleza kwamba: "watoto wa Kipalestina daima wamekuwa ni jinamizi kwa Wazayuni."
Katika jibu ililotoa kwa madhila ya zaidi ya miongo saba ya kukaliwa kwa mabavu Palestina na zaidi ya miaka kumi na tano ya kuwekewa mzingiro Gaza na kufungwa jela na kuteswa maelfu ya Wapalestina, mnamo tarehe 7 Oktoba, Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas) ilianzisha operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa.
Operesheni hiyo inachukuliwa kuwa moja ya mashambulio makali zaidi dhidi ya utawala dhalimu wa Kizayuni. Wapiganaji wa Hamas walipenya kwenye maeneo yanayokaliwa kwa mabavu kupitia nukta kadhaa za uzio wa mpakani na kushambulia vijiji kadhaa, ambapo mbali na kuangamiza idadi kubwa ya Wazayuni, waliwakamata mateka wengine kadhaa miongoni mwao.
Ili kufidia kushindwa kwake katika operesheni za Muqawama, tokea Oktoba 7 hadi sasa utawala wa Kizayuni umekuwa ukifanya mashambulio ya kinyama na ya mtawalia dhidi ya maeneo tofauti ya Ukanda wa Gaza; na matokeo yake Wapalestina zaidi ya elfu kumi wameshauawa shahidi hadi sasa na wengine wasiopungua elfu 27 wamejeruhiwa.../