-
Mashindano ya 39 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yafunguliwa rasmi mjini Tehran
Feb 19, 2023 01:32Mashindano ya 39 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yamefunguliwa rasmi Jumamosi alasiri mjini Tehran.
-
Ebrahim Raisi: Taifa la Iran limesambaratisha njama za maadui kwa 'istiqama' ya kupigiwa mfano
Feb 18, 2023 22:56Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, taifa la Iran limefanikiwa kusambaratisha njama za maadui kwa muqawama na istiqama ya kupigiwa mfano.
-
Kiongozi Muadhamu azikosoa nchi za Waislamu kwa kufumbia macho kadhia ya Palestina
Feb 18, 2023 07:28Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amezikosoa nchi za Kiislamu kwa kutochokua hatua yoyote ya maana juu ya kadhia ya Palestina.
-
Iran yamshambulia Macron kwa kukutana na wanaopinga Mapinduzi ya Kiislamu
Feb 18, 2023 06:49Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amemjia juu Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa kwa kukutana na 'shakhsia' wanaopinga mfumo wa uongozi na Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran tokeo mwaka 1979.
-
Kan'ani Chafi: Muda si mrefu maadui wataipigia magoti Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
Feb 18, 2023 04:09Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, muda si mrefu maadui wa Iran watalazimika kulipigia magoti taifa hili na kusalimu amri mbele yake kutokana na kusimama kidete, nguvu na adhama ya taifa hili.
-
Imamu wa Swala ya Ijumaa Tehran akosoa mienendo ya Wamagharibi kuhusu tetemeko la ardhi nchini Syria
Feb 17, 2023 10:02Imam wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amekosoa mienendo ya nchi za Magharibi kuhusiana na tetemeko la ardhi nchini Syria.
-
Sisitizo la Kiongozi Muadhamu juu ya ulazima wa kuongezwa nguvu za kiulinzi za nchi
Feb 17, 2023 06:57Katika miaka ya baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, maendeleo ya kiulinzi ya Iran ambayo yamepatikana kwa kutegemea elimu na wataalamu wa hapa ndani yamefikia katika kiwango ambacho kimewakasirisha mno maadui wa taifa hili la Kiislamu.
-
Iran yatoa jibu kwa taarifa ya pamoja ya US na Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi
Feb 17, 2023 04:23Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ametupilia mbali maelezo yaliyomo kwenye taarifa ya kikao cha tatu cha jopo kazi la pamoja la Marekani na Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi (GCC) kuhusu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na kueleza kwamba kutolewa taarifa kama hiyo kunaendana na mkakati wa muda mrefu wa utawala wa Marekani wa kuzusha mfarakano kati ya nchi za eneo hili.
-
Amir-Abdollahian: Madai ya Marekani ya kumhusisha kiongozi wa Al-Qeada na Iran yanachekesha
Feb 16, 2023 23:43Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amejibu madai ya msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani na kusema: "Utungaji habari kuhusiana na kiongozi wa Al-Qaeda na kumhusisha yeye na Iran ni jambo la kuchekesha."
-
Iran na US katika 'mazungumzo' ya kubadilishana wafungwa
Feb 16, 2023 23:21Marekani na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zipo katika mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja juu ya suala la kubadilishana wafungwa, huku Qatar na Uingereza zikiwa wapatanishi kwenye mazungumzo hayo.