Feb 18, 2023 10:19 UTC
  • Iran yamshambulia Macron kwa kukutana na wanaopinga Mapinduzi ya Kiislamu

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amemjia juu Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa kwa kukutana na 'shakhsia' wanaopinga mfumo wa uongozi na Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran tokeo mwaka 1979.

Katika ujumbe aliotuma kwenye mtandao wa Twitter leo Jumamosi, Nasser Kanani amesema kufanya mikutano ya aina hiyo inadhihirisha upumbavu na upofu wa miaka 44 wa kutoona namna wananchi wa Iran wanavyoiunga mkono nchi yao, Mapinduzi na Uongozi.

Amewataja shakhsia waliokutana na Macron hivi karibuni na pia mwezi Novemba mwaka uliopita kama vikaragosi na vibaraka wasio na hadhi wala heshima.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameeleza bayana kuwa, Rais wa Ufaransa haamini misingi ya demokrasia, na ameshindwa kuwa na ufahamu na kulitambua taifa la Iran na Mapinduzi ya Kiislamu.

Kabla ya hapo alisema muda si mrefu maadui wa Iran watalazimika kulipigia magoti taifa hili na kusalimu amri mbele yake kutokana na kusimama kidete, nguvu na adhama ya taifa hili.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran

Kanaani ameashiria kutoalikwa Iran kwa ajili ya kushiriki katika mkutano wa usalama wa Munich na kueleza kuwa maana yake ni kukosea katika mahesabu na kuendeleza mwenendo ule ule wa kisiasa wenye makosa.

Ameongeza kwamba, wale ambao kwa miaka 44 sasa wanafumbia macho ushiriki mkubwa na usio na mithili wananchi wa Iran katika kuunga mkono Mapinduzi ya Kiislamu na Kiongozi wake.

Tags