-
Rais wa Iran kuelekea China kwa ziara rasmi
Feb 12, 2023 03:52Kwa kuitikia mwaliko rasmi wa Rais Xi Jinping wa China, rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Ebrahim Raisi kesho Jumatatu anatazamiwa kuelekea mji mkuu wa China Beijing.
-
Abdollahian: Wairani wametoa jibu kwa maadui kwa maadamano ya Bahman 22
Feb 11, 2023 23:04Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kushiriki kwa wingi wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu kwenye maandamano ya Bahman 22 ya kuadhimisha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni jibu zito la Wairani kwa maadui wa taifa hili.
-
Rais Raisi: Adui hawezi kuyavumilia maendeleo ya Iran
Feb 11, 2023 08:27Rais Ebrahim Raisi amesema kuhusiana na mafanikio yaliyopatikana nchini katika nyuga mbalimbali za sayansi, teknolojia, uchumi, ulinzi, afya na tiba kwamba adui hawezi kuyavumilia maendeleo na hatua ilizopiga Iran.
-
Azimio la Bahman 22: Kuwa kitu kimoja, mkakati muhimu zaidi wa Wairan wa kumshindia adui
Feb 11, 2023 08:27Wananchi wa Iran wametangaza katika azimio lao walilotoa mwishoni mwa maandamano ya Bahman 22 ya kwamba, kuwa kitu kimoja, kuungana, mshikamano, umoja wa kitaifa, kuwa na moyo mmoja makundi na matabaka na kushirikiana watu wa kaumu na dini zote nchini ni wajibu wa kidini na kimapinduzi na ndio mkakati muhimu zaidi wa kumshindia adui.
-
Kuboreshwa uwezo wa ndege zisizo na rubani za Jeshi la Anga la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
Feb 11, 2023 05:49Brigedia Jenerali Hamid Vahedi, Kamanda wa Jeshi la Anga la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, amewasilisha ripoti ya utendaji wa mwaka jana wa jeshi hilo na kutangaza ongezeko la 33% la idadi ya ndege zisizo na rubani za Jeshi la Anga.
-
Wairani washiriki kwa wingi katika maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu
Feb 11, 2023 04:26Sherehe za ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini zimeanza mapema leo kote nchini kwa ajili ya kuadhimisha miaka 44 ya mapinduzi hayo hayo, huku miji na vijiji vyote vya Iran vikishuhudia maandamano makubwa kuelekea viwanja na maeneo ya umma.
-
Wairani kuadhimisha Mapinduzi ya Kiislamu leo, sauti za Takbira zatanda kote nchini kuanzia jana usiku
Feb 10, 2023 23:36Wananchi wa Iran leo wanatarajiwa kushiriki kwa wingi katika maandamano ya maadhimisho ya miaka 44 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kupiga nara dhidi ya Marekani na madola mengine ya kibeberu.
-
Raisi: Iran iko tayari kwa makubaliano kuhusu JCPOA lakini Marekani na E3 zilifanya makosa
Feb 10, 2023 23:02Rais wa Iran Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza utayarifu wa Tehran kufikia makubaliano "ya haki" ya mwisho kwa lengo la kufufua makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015 yaliyotelekezwa na Marekani, akisema hata hivyo, Marekani na washirika wake wa Ulaya wanajihadaa na walifanya makosa kwa kuamua kuingilia masuala ya ndani ya Iran.
-
Ayatullah Khatami: Matembezi ya Bahman 22 ni ishara ya ushindi wa wananchi dhidi ya njama zote
Feb 10, 2023 07:42Khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa ya mjini Tehran amesema kuwa, matembezi ya Bahman 22 (Febrauri 11) ambayo yatafanyika kesho Jumamosi katika kona zote za Iran kuadhimisha mwaka wa 44 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, kwa taufiki na uwezo wa Mwenyezi Mungu yatakuwa ni muhuri wa ushindi wa wananchi wa Iran ya Kiislamu dhidi ya njama zote za maadui.
-
Shehena ya sita ya misaada ya Iran yawafikia wahanga wa tetemeko la ardhi nchini Syria
Feb 10, 2023 07:00Shehena ya sita ya ndege ya misaada ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa ajili ya wahanga wa tetemeko la ardhi imewafikia wananchi wa Syria mapema leo Ijumaa.