Abdollahian: Wairani wametoa jibu kwa maadui kwa maadamano ya Bahman 22
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i93940-abdollahian_wairani_wametoa_jibu_kwa_maadui_kwa_maadamano_ya_bahman_22
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kushiriki kwa wingi wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu kwenye maandamano ya Bahman 22 ya kuadhimisha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni jibu zito la Wairani kwa maadui wa taifa hili.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 11, 2023 23:04 UTC
  • Abdollahian: Wairani wametoa jibu kwa maadui kwa maadamano ya Bahman 22

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kushiriki kwa wingi wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu kwenye maandamano ya Bahman 22 ya kuadhimisha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni jibu zito la Wairani kwa maadui wa taifa hili.

Hossein Amir-Abdollahian, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran alisema hayo jana Jumamosi katika mahojiano na shirika la habari la Iran Press pambizoni mwa maadhimisho ya mwaka wa 44 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kusisitiza kuwa, "Wananchi (wa Iran) daima wanaiunga mkono serikali, nao ndio nguvu yetu kubwa yenye thamani." 

Hapo jana, mamilioni ya Wairani walishiriki katika sherehe hizo za tarehe 22 Bahman (Februari 11) ili kusisitiza mshikamano wao mkubwa, kizazi baada ya kizazi, na thamani za Mapinduzi ya Kiislamu, wakipeperusha bendera ya Uislamu na kuzidisha matumaini ya kupata ushindi watu wote wanaokandamizwa na kudhulumiwa duniani.

Matembezi ya Bahman 22

Maadhimisho ya Bahman 22 yanajiri baada ya kufeli njama kubwa iliyoanzishwa na madola ya kigeni dhidi ya Iran ya Kiislamu katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita, iliyolenga usalama wa ndani na umoja na mshikamano wa taifa kwa kuibua ghasia na kuziunga mkono kupitia vita mseto vya kisiasa, kiuchumi na hujuma ya vyombo vya habari vya Magharibi.

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameeleza bayana kuwa, "Jukumu letu katika serikali ni kuwaandalia wananchi mazingira na hali nzuri, na tumejitolea kwa dhati kuliafiki hilo."