-
Velayati: Uhusiano wa Iran na Russia ni wa kina, wa kimkakati na unaostawi
Jan 05, 2023 06:20Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa amesema kwamba uhusiano wa Iran na Russia hivi sasa uko katika kiwango bora zaidi na unaendelea kustawi.
-
Rdiamali ya Waziri wa Utamaduni wa Iran kwa hatua ya udhalilishaji ya jarida la Kifaransa
Jan 05, 2023 05:49Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu wa Iran ametoa radiamali yake kupitia ukurasa wake wa kijamii kuhusu hatua ya dharau na udhalilishaji iliyochukuliwa karibuni na jarida la Ufaransa la Charlie Hebdo dhidi ya Ayatullah Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
-
Raisi: Mafanikio ya sekta ya anga za mbali ya Iran ni ithibati ya kufeli kwa vikwazo
Jan 05, 2023 03:49Rais wa Iran amesema mafanikio ya Jamhuri ya Kiislamu katika sekta ya anga za mbali ni ishara tosha ya kufeli na kugonga mwamba vikwazo vya Wamagharibi na njama zao za kutaka kulitenga taifa hili.
-
Yemen: Israel inastahili kusambaratishwa na kufutwa katika eneo
Jan 05, 2023 03:30Balozi wa Yemen mjini Tehran amesema kila mtu ana jukumu na nafasi katika harakati ya muqawama, na jukumu lenyewe ni kutia nguvu jitihada za kuitimua Marekani katika eneo hili la Asia Magharibi, na kuufuta utawala haramu wa Israel katika eneo.
-
Mtazamo wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusu dhulma za mfumo wa ubepari wa Magharibi kwa wanawake
Jan 05, 2023 02:01Ubepari wa Magharibi na demokrasia ya kiliberali, ambayo baada ya kuanguka kwa Umoja wa Kisovieti mnamo 1991, kulingana na wanafikra wengine wa Magharibi kama vile Francis Fukuyama, iliushinda mfumo wa kikomunisti kama mfumo bora wa kisiasa na kiuchumi, na kutambuliwa kama mwisho wa historia, sasa unakabiliwa na matatizo makubwa na ya kimsingi.
-
Iran yamuita balozi wa Ufaransa kulalamikia uafriti wa 'Charlie Hebdo'
Jan 05, 2023 00:01Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imemuita balozi wa Ufaransa mjini Tehran, Nicolas Roche kulalamikia vikali kitendo cha jarida la Kifaransa cha kutukana na kuvunjia heshima matukufu ya Kiislamu na thamani za kitaifa na kidini za Jamhuri ya Kiislamu.
-
Kiongozi wa Mapinduzi: Magharibi imemdhulumu mwanamke na kukanyaga hadhi na utu wake
Jan 04, 2023 10:00Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameutaja msimamo wa Jamhuri ya Kiislamu mkabala wa wanaodai kinafiki kuwa wanatetea haki za wanawake wa Kimagharibi kuwa ni wa kudai na kuhujumu na akasema kuwa, Magharibi ya kisasa na utamaduni ulioporomoka wa Magharibi vina hatia katika suala hili na wametenda makosa na uhalifu dhidi ya utu na hadhi ya mwanamke.
-
Ammar Hakim: Kosa la Marekani la kuwauwa makamanda wa muqawama halisameheki
Jan 04, 2023 04:04Sayyid Ammar Hakim, Kiongozi wa Harakati ya Hikma ya Kitaifa ya Iraq amesema kuwa, kosa la Marekani la kuwauwa makamanda wa ushindi wa muqawama halisameheki.
-
Israel yaonywa na kutakiwa iache chokochoko zake dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
Jan 04, 2023 04:03Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa ameuonya utawala haramu wa Israel na kuutaka uachane na chokochoko zake za kijeshi dhidi ya taifa hili ambazo zina lengo la kutekeleza sera zake za kishari katika eneo la Asia Magharibi.
-
Msemaji wa Mahakama ya Iran: Kuna washtakiwa 154 katika kesi ya Shahidi Soleimani
Jan 04, 2023 01:01Msemaji wa Mahakama ya Iran amesema: "Washtakiwa 154 wametambuliwa katika kesi ya mauaji ya makamanda wa muqawama na miongoni mwa washtakiwa hao kuna Wamarekani 96 huku mchakato wa uchunguzi ukiendelea."