Jan 04, 2023 07:34 UTC
  • Ammar Hakim: Kosa la Marekani la kuwauwa makamanda wa muqawama halisameheki

Sayyid Ammar Hakim, Kiongozi wa Harakati ya Hikma ya Kitaifa ya Iraq amesema kuwa, kosa la Marekani la kuwauwa makamanda wa ushindi wa muqawama halisameheki.

Sayyid Ammar Hakim amesema hayo katika hauli na kumbukumbu ya mwaka tatu wa kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa kamanda wa kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzii wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) na  Abu Mahdi al Muhandis, aliyekuwa Naibu Mkuu wa harakati ya kujitolea ya wananchi wa Iraq ya Hashd al Sha'abi na wanamapambano wengine wanane.

Kiongozi wa Harakati ya Hikma ya Kitaifa ya Iraq amesisitiza kuwa, jinai ya kutisha iliyofanywa dhidi ya makamanda hao wa ushindi lilikuwa kosa la Marekani kwa wananchi wa Iraq na wageni wao ambao walijitolea mno na kupelekea kupatikana ushindi, hivyo ni kkosa ambao kwa hakika halisameheki.

Aidha ameongeza kuwa: Daima tunapaswa kukumbusha na kuthamini misimamo ya kihistoria ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa uongozi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei katika ushindi wa wananchi wa Iraq na kusimama pamoja nao sambamba na kuwahami katika vita dhidi ya ugaidi wa Daesh.

Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH, aliuawa shahidi Januari 3, 2020 katika shambulio la anga lililofanywa na jeshi vamizi na la kigaidi la Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad, akiwa pamoja na Abu Mahdi al Muhandis, Naibu Mkuu wa harakati ya kujitolea ya wananchi wa Iraq ya al Hashd al Sha'abi na wanamapambano wengine wanane, wakati alipoelekea Iraq kwa mwaliko rasmi wa serikali ya nchi hiyo.

Tags