Kallas: Estonia inaipiku Marekani katika uhuru wa kujieleza
https://parstoday.ir/sw/news/world-i136688-kallas_estonia_inaipiku_marekani_katika_uhuru_wa_kujieleza
Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya, Kaja Kallas amepuuzilia mbali ukosoaji wa Washington kuhusu mbinyo wa kutoa maoni katika nchi wanachama wa umoja huo, akisisitiza kwamba nchi yake ya asili ya Estonia ina uhuru mkubwa zaidi wa kujieleza kuliko Marekani.
(last modified 2026-02-16T10:11:48+00:00 )
Feb 16, 2026 10:11 UTC
  • Kallas: Estonia inaipiku Marekani katika uhuru wa kujieleza

Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya, Kaja Kallas amepuuzilia mbali ukosoaji wa Washington kuhusu mbinyo wa kutoa maoni katika nchi wanachama wa umoja huo, akisisitiza kwamba nchi yake ya asili ya Estonia ina uhuru mkubwa zaidi wa kujieleza kuliko Marekani.

Wakati wa majadiliano ya wazi katika Mkutano wa Usalama wa Munich, Kallas aliombwa kutoa radimali yake kwa ukosoaji wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio kuhusu kuzidi kuwa mbaya uhuru wa kujieleza barani Ulaya.

Akijibu tuhuma hizo, mwanadiplomasia huyo wa EU amesema, "Kama mtu anayetoka katika nchi ambayo iko katika nafasi ya pili katika Orodha ya Uhuru wa Vyombo vya Habari, kusikia ukosoaji wa uhuru wa vyombo vya habari kutoka kwa nchi ambayo iko nafasi ya 58 katika orodha hii, inashangaza." Kwa mujibu wa orodha ya hivi karibuni ya Wanahabari Wasio na Mipaka, Estonia iko katika nafasi ya pili duniani; huku Marekani ikiwa katika nafasi ya 57.

Rubio wakati wa hotuba yake huko Munich Jumamosi, alionya dhidi ya kile alichokielezea kama mitindo ya kisiasa na kitamaduni inayodhoofisha ustaarabu wa Magharibi na kupungua kwa 'idiolojia' ndani ya taasisi za Ulaya.

Brussels imekabiliwa na ukosoaji kwa muda mrefu kuhusu udhibiti mkubwa wa maudhui mitandaoni, ikiwa ni pamoja na Sheria ya Huduma za Kidijitali ya 2022 (DSA), ambayo inaweka masharti makali ya udhibiti kwenye majukwaa makubwa.

Washington imeishutumu EU kwa kutumia sheria hiyo kukandamiza uhuru wa kujieleza na kuwadhibiti watumiaji wa mitandao ya kijamii ya Marekani.