Yemen: Israel inastahili kusambaratishwa na kufutwa katika eneo
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i92516-yemen_israel_inastahili_kusambaratishwa_na_kufutwa_katika_eneo
Balozi wa Yemen mjini Tehran amesema kila mtu ana jukumu na nafasi katika harakati ya muqawama, na jukumu lenyewe ni kutia nguvu jitihada za kuitimua Marekani katika eneo hili la Asia Magharibi, na kuufuta utawala haramu wa Israel katika eneo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 05, 2023 03:30 UTC
  • Yemen: Israel inastahili kusambaratishwa na kufutwa katika eneo

Balozi wa Yemen mjini Tehran amesema kila mtu ana jukumu na nafasi katika harakati ya muqawama, na jukumu lenyewe ni kutia nguvu jitihada za kuitimua Marekani katika eneo hili la Asia Magharibi, na kuufuta utawala haramu wa Israel katika eneo.

Ibrahim Mohammad al-Deilami amesema hayo katika Kongamano la Kwanza la Kimataifa la kumbukumbu ya kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa kamanda wa kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzii wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC.

Mohammad al-Deilami amesisitiza kuwa, "Tunapaswa kujenga umoja wa harakati ya muqawama, ili kusambaratisha njama za maadui wanaofanya hujumu dhidi ya utamaduni; tunapaswa kuwa na uongozi na sera."

Mwanadiplomasia huyo wa Yemen hapa Tehran ameeleza bayana kuwa, 'Lazima tuimarishwe uwepo wetu katika nchi za Kiarabu na Kiislamu, ili tuondokane na uwepo wa maadui katika eneo hili."

Al-Delaimi amesisitiza kuwa, kila mmoja ana wajibu wa kushajiisha na kupiga jeki jitihada za kuhakikisha kuwa Marekani inaondoka katika eneo hili la kistratajia la Asia Magharibi, sambamba na kuufuta utawala haramu wa Israel katika eneo.  

Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC, aliuawa shahidi Januari 3, 2020 katika shambulio la anga lililofanywa na jeshi vamizi na la kigaidi la Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad.

Aliuawa shahidi akiwa pamoja na Abu Mahdi al Muhandis, aliyekuwa Naibu Mkuu wa harakati ya kujitolea ya wananchi wa Iraq ya al Hashd al Sha'abi na wanamapambano wengine wanane, wakati alipoelekea Iraq kwa mwaliko rasmi wa serikali ya nchi hiyo.