-
Amir-Abdollahian: Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq alikuwa amebeba salamu za Marekani kwa Iran
Sep 30, 2022 04:29Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema, katika kipindi cha miezi iliyopita baadhi ya mawaziri wa mambo ya nje wa nchi kadhaa wamekuwa wakifikisha jumbe za Marekani kwa Iran na kinyume chake, na akaongeza kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq, Fuad Hussein naye pia alikuwa amebeba ujumbe wa salamu za Marekani kwa Iran.
-
IRGC yashambulia kwa makombora ya balestiki ngome za magaidi kaskazini mwa Iraq
Sep 29, 2022 08:36Vikosi vya Nchi Kavu vya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) vimeanzisha duru mpya ya mashambulio dhidi ya ngome na maficho ya magaidi kwa kutumia makombora ya balestiki huko kaskazini mwa Iraq.
-
Undumakuwili wa nchi za Magharibi kuhusiana na haki za binadamu nchini Iran
Sep 29, 2022 08:27Huku Wamagharibi wakiendelea kuwachochea wananchi wa Iran kufanya ghasia na maandamano yenye uharibu, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani misimamo na mienendo ya kindumakuwili ya nchi za Magharibi mkabala wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na haki za binadamu.
-
Raisi: Matakwa ya Iran kwenye mazungumzo ni kuhakikishiwa dhamana ya kuaminika
Sep 29, 2022 04:39Rais wa Iran amesisitiza kuhusu dhamana yenye kuaminika na kupatia ufumbuzi masuala ya kiusalama kwa lengo la kuzuia kukiukwa tena utendaji na majukumu ya pande za Magharibi na kutolewa azimio dhidi ya Iran kwa visingizio vya kisiasa vya kiusalama.
-
Iran: Jitihada za kufelisha kabisa vikwazo vya mabeberu zinaendelea
Sep 28, 2022 07:18Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa, juhudi zinaendelea za kuhakikisha vikwazo vya mabeberu dhidi ya taifa hili la Kiislamu vinafeli na kutokuwa na athari yoyote.
-
Jen. Safavi: Sera ya muqawama inazidi kuimarika na kupata nguvu
Sep 28, 2022 04:47Mshauri Mkuu wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, stratejia ya muqawama katika eneo hili la Asia Magharibi na miongoni mwa mataifa yanayopenda haki duniani inazidi kuimarika na kupata nguvu, na bila shaka nguvu hizo zitafelisha njama za kambi ya ubeberu.
-
"Ni kinaya kwa wenye uraibu wa vikwazo kudai wanawahurumia Wairani"
Sep 28, 2022 04:44Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amekosoa undumakuwili wa Marekani ambayo inadai kuwa ina huruma na mapenzi na wananchi wa Iran, wakati ambapo imeliwekea taifa hili vikwazo shadidi.
-
Amir Abdollahian: Tupo tayari kujibu maswali ya wakala wa IAEA
Sep 28, 2022 01:14Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa Tehran iko tayari kujibu maswali ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia (IAEA) hata hivyo ameongeza kwamba wakala huo unapasa kutekeleza wajibu wake wa kiufundi.
-
Kubadilishwa ghafla faili la kesi ya Mahsa Amini kuwa mradi wa mapinduzi dhidi ya serikali
Sep 27, 2022 22:48Kwa kuzingatia kuwa utawala haramu wa Israel uliamuru hadharani kuuawa kigaidi Shirin Abu Akleh, mwandishi wa habari wa Kipalestina wa televisheni ya al-Jazeera, Mkristo ambaye pia alikuwa na uraia wa Marekani akiwa kazini huko Jenin, na ambapo umeshindwa kuhalalisha kitendo hicho, hivyo umeamua kukaa kimya kwa sasa kuhusu kifo cha Mahsa Amini.
-
"Magharibi inafanya njama za kufuta matukufu ya Kiislamu na kupandikiza upotofu wake"
Sep 27, 2022 07:21Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amendelea na harakati zake za kidiplomasia pembeni mwa kikao cha 77 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa kuonana na kufanya mazungumzo na mawaziri wenzake wa mambo ya nje kuanzia wa mashariki hadi magharibi mwa Asia na kutoka Amerika ya Latini hadi Ulaya na Afrika.