Raisi: Matakwa ya Iran kwenye mazungumzo ni kuhakikishiwa dhamana ya kuaminika
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i88698-raisi_matakwa_ya_iran_kwenye_mazungumzo_ni_kuhakikishiwa_dhamana_ya_kuaminika
Rais wa Iran amesisitiza kuhusu dhamana yenye kuaminika na kupatia ufumbuzi masuala ya kiusalama kwa lengo la kuzuia kukiukwa tena utendaji na majukumu ya pande za Magharibi na kutolewa azimio dhidi ya Iran kwa visingizio vya kisiasa vya kiusalama.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 29, 2022 04:39 UTC
  • Raisi: Matakwa ya Iran kwenye mazungumzo ni kuhakikishiwa dhamana ya kuaminika

Rais wa Iran amesisitiza kuhusu dhamana yenye kuaminika na kupatia ufumbuzi masuala ya kiusalama kwa lengo la kuzuia kukiukwa tena utendaji na majukumu ya pande za Magharibi na kutolewa azimio dhidi ya Iran kwa visingizio vya kisiasa vya kiusalama.

Rais Ayatullah Sayyid Ebrahim Raeisi wa Iran jana usiku alizungumza na wananchi mubashara kwa njia ya televisheni; ambapo aliulizwa swali kuhusu mchakato unaoendelea sasa kuhusu faili la nyuklia na kuashiria mazungumzo ya karibuni kati yake na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na kusema, katika mazungumzo hayo alitilia mkazo juu ya masuala mawili muhimu ambayo ni kutatuliwa masuala ya kiusalama na kuondoa kabisa vikwazo kwa manufaa ya kiuchumi ya taifa la Iran. 

Rais wa Iran (kulia) mjini New York na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron 

Rais Raisi aidha amekosoa mienendo ya matamshi ya kisiasa ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia (IAEA) na kusema, maafisa wa wakala huo baada ya kukagua na kuchunguza hali ya kinyuklia ya Iran wametangaza rasmi kwamba hakuna ukengeukaji wowote ulioshuhudiwa hapa nchini hata hivyo mara wanaporejea Ulaya au kuwasiliana na utawala wa Kizayuni lugha na matamshi yao hubadilika; suala linaloashiria namna pande hizo zinavyolitazama suala hilo kisiasa. 

Ayatullah Raisi  ameeleza kuwa, Iran imeunganishwa na miundo mbinu ya kiuchumi ya Asia kwa kuwa mwanachama katika Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai; na kusisitiza kuwa raia katika nchi wanachama wa Shanghai wanaunda sehemu kubwa ya jamii ya watu wote duniani; na nchi hizi ni sehemu muhimu ya uchumi wa dunia.   

Akijibu swali kuhusu tukio la Mahsa Amini ambalo lilijiri sambamba na ziara yake huko Samarkand nchini Uzbekistan na hatua zilizochukuliwa hadi sasa kuweka wazi suala hili, Ayatullah Rais pia ameibu kwa kusema: "Msingi wetu katika kadhia hii ya kifo cha Mahsa Amini ni uwazi na uadilifu. Kama kulikuwa na upuuzaji na makosa katika kadhia hii tambua kuwa suala hilo litafuatiliwa kikamilifu."