Amir Abdollahian: Tupo tayari kujibu maswali ya wakala wa IAEA
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i88650-amir_abdollahian_tupo_tayari_kujibu_maswali_ya_wakala_wa_iaea
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa Tehran iko tayari kujibu maswali ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia (IAEA) hata hivyo ameongeza kwamba wakala huo unapasa kutekeleza wajibu wake wa kiufundi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 28, 2022 01:14 UTC
  • Amir Abdollahian: Tupo tayari kujibu maswali ya wakala wa IAEA

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa Tehran iko tayari kujibu maswali ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia (IAEA) hata hivyo ameongeza kwamba wakala huo unapasa kutekeleza wajibu wake wa kiufundi.

Hossein Amir- Abdollahian amesema: Tutaimarisha ushirikiano na IAEA iwapo wakala huo utazingatia wajibu na utendaji wake wa kiufundi. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameongeza kuwa: Marekani na nchi tatu za Ulaya zimefanya makosa. Nchi hizo ziliwasilisha azimio wakati tukiendelea na mazungumzo. Amir- Abdollahian ameeleza kuwa tatizo ililonalo Iran kwa wakala wa IAEA ni hili kwamba, chombo hicho kinafanya kazi kwa mujibu wa matashi ya kisiasa.  

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameongeza kuwa, asilimia mbili ya shughuli za nyuklia duniani zinafanywa nchini Iran tena katika mfumo wa amani hata hivyo wakala huo unaifanyia Iran ukaguzi kwa asilimia 37. 

Kuhusu mazungumzo ya Iran na Saudi Arabia, Amir Abdollahian ameashiria duru tano za mazungumzo na kusema: Nchi mbili zimekubaliana juu ya masuala kadhaa na tunakaribisha kurejea uhusiano wa kidiplomasia wa nchi mbili katika hali ya kawaida na kufunguliwa tena balozi za nchi mbili." Tumeacha mlango wazi kwa Saudia kurejea katika uhusiano wa kawaida na Iran."

Iran na Saudia katika juhudi za kuhuisha uhusiano kati yazo 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amegusia pia kuhusu ushirikiano wa kiulinzi kati ya Iran na Russia na kueleza kuwa nchi mbili zinashirikiana kiulinzi hata hivyo amesema Iran haiungi mkono upande wowote katika vita huko Ukraine na inapinga vita hivyo.