-
Maimamu wa Ijumaa Iran: SEPAH ni mwiba kwa adui na tumaini kwa Waislamu wote
Apr 22, 2022 22:24Maimamu wa Sala za Ijumaa zilizosaliwa jana kote nchini Iran walisema katika khutba zao kuwa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH ni mwiba katika macho ya maadui na ni tumaini jema kwa kila Muislamu ulimwenguni.
-
Waafghani wote walioko Iran wamepokea chanjo ya bure ya COVID-19
Apr 22, 2022 22:05Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema raia wote wa Afghanistan wanaoshi kama wakimbizi hapa nchini wamepigwa chanjo ya kupambana na ugonjwa wa COVID-19 bila malipo.
-
Khatibu wa Sala ya Ijumaa: Maandamano ya Siku ya Quds yanamtia kiwewe adui Mzayuni
Apr 22, 2022 07:00Khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa ya hapa jijini Tehran amesisitizia wajibu wa kujitokeza kwa wingi wananchi wa Iran katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds ambayo ni Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani na kusema kuwa, maandamano hayo yanamtia kiwewe adui.
-
Sisitizo la Iran la kurudishwa amani ya kudumu katika eneo kwa kuondolewa ukaliwaji mabavu wa ardhi za Palestina
Apr 22, 2022 03:46Hussein Amir Abdollahian, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa amani ya kudumu katika eneo la Asia Magharibi itapatikana tu kwa kuondolewa kikamilifu ukaliwaji mabavu wa ardhi za Palestina, kurejea wakimbizi wote katika ardhi zao za jadi na kuainishwa mfumo wa utawala wa baadaye wa Palestina kwa msingi wa kura ya maoni pamoja na kuundwa serikali huru katika ardhi hizo.
-
Al-Jazeera: Iran imeionya Israel, yaiambia maghala yako ya silaha yatalengwa
Apr 22, 2022 02:41Televisheni ya Al-Jazeera ya Qatari imeripoti kuwa, Iran imetuma picha na ramani za maghala ya silaha za nyuklia za utawala wa Kizayuni kwa serikali ya Tel Aviv kupitia nchi moja ya Ulaya.
-
Iran yavunja rekodi yake ya kusafirisha bidhaa barani Afrika, Kenya na Tanzania zimo
Apr 21, 2022 21:22Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Masuala ya Kiarabu na Kiafrika ya Shirika la Ustawi wa Biashara la Iran amesema kuwa, kiwango cha usafirishaji bidhaa za Iran kuelekea barani Afrika uongezeka kwa asilimia 107 na kuvunja rekodi yake ya huko nyuma.
-
Ayatullah Hamedani: Wanaodai kutetea haki za binaadamu duniani wamefedheheka tena
Apr 21, 2022 07:39Ayatullah Nouri Hamedani ambaye ni miongoni mwa viongozi wakuu wa kidini katika mji mtakatifu wa Qum nchini Iran amelaani kitendo cha kuvunjiwa heshima kitabu kitukufu cha Mwenyezi Mungu, Qur'ani huko Sweden na Msikiti wa al Aqsa huko Quds Tukufu na vilevile mauaji ya watu wa Afghanistan.
-
Iran: Kimya cha kimataifa kimechochea jinai za Israel dhidi ya Palestina
Apr 21, 2022 03:48Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Hossein Amir-Abdollahian, amesema undumakuwili na kimya cha baadhi ya serikali na duru za kimataifa ndio chanzo cha kupata ubavu Israel katika kuzidisha uvamizi dhidi ya Wapalestina na ukiukaji wa haki zao.
-
Iran yawakamata majasusi watatu wa Mossad
Apr 21, 2022 03:35Wizara ya Usalama wa Taifa ya Iran imetangaza kuwakamata majasusi watatu waliokuwa wakitumikia shirika la ujasusi la Israel, Mossad, katika mkoa wa Sistan na Baluchestan, Kusini Magharibi mwa nchi.
-
Amali za usiku wenye fadhila wa Laylatul Qadr zafanyika katika Iran ya Kiislamu
Apr 20, 2022 22:45Amali za usiku mtukufu wa kwanza wa Laylatul Qadr zimefanyika katika pembe zote za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambapo umati mkubwa wa waumini umeshiriki ibada za usiku huu mtukufu huku waumini wakizingatia kanuni za kuzuia maambukizi ya corona.