-
Jeshi la Iran lazindua trela ya kubeba vifaru iliyoundwa nchini
Apr 20, 2022 06:40Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limezindua trela ndefu yenye uwezo wa kubebe vifaru ambayo imeundwa kikamilifu na wataalamu wa Iran.
-
Rais wa Iran alaani hujuma ya kigaidi Afghanistan
Apr 20, 2022 06:29Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani hujuma ya kigaidi dhidi ya shule kadhaa katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul sambamba na kutuma salamu za rambirambi kwa familia za waliopoteza maisha.
-
Iran na Mauritania zahimiza kuimarisha ushirikiano wao katika nyuga zote
Apr 20, 2022 03:18Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amefanya mazungumzo ya simu na waziri mwenzake wa mambo ya nje wa Mauritania na kutilia mkazo udharura wa kuimarishwa uhusiano wa Tehran na Nouakchott katika nyuga zote.
-
SEPAH: Adui ana kiwewe kikubwa kwa kuona mshikamano katika majeshi ya Iran
Apr 19, 2022 22:43Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH amesema wakati alipoonana na Kamanda Mkuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu kwamba umoja na mshikamano wa vikosi vya ulinzi vya Iran unamtia kiwewe adui.
-
Mshauri wa Rais wa Iran: Kuvunjia heshima matukufu ya watu ni kuchochea machafuko
Apr 19, 2022 06:18Mshauri wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kitendo cha nchi za Magharibi cha kuruhusu kuvunjiwa heshima matukufu ya dini za watu wachache katika nchi hizo ni fitna kubwa inayopanda mbegu ya machafuko.
-
Kenya na Iran kuimarisha uhusiano wao katika nyuga za utalii na uwekezaji
Apr 19, 2022 03:38Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Kenya zimeazimia kusaini makubaliano ya maelewano juu ya kuimarisha uhusiano wa pande mbili katika nyuga za uwezekaji na utalii.
-
Drone "Gaza" ya Jeshi la Sepah la Iran yafaulu majaribio na kuanza kufanya kazi kikamilifu
Apr 18, 2022 22:30Ndege mpya isiyo na rubani ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) iliyopewa jina la Gaza, imefaulu majaribio ya kuruka na sasa inafanya kazi kikamilifu.
-
Usafirishaji wa bidhaa za Iran nchini Afrika Kusini waongezeka kwa asilimia 500
Apr 18, 2022 21:44Mkuu wa Shirika la Ustawi wa Kibiashara la Iran limetangaza kuwa, usafirishaji nje bidhaa za Iran umepindukia dola bilioni 13 huku nchi za Afrika Kusini na Ghana zikiongoza kwa barani Afrika.
-
Raisi aionya Israel isithubutu kuichokoza Iran hata kidogo
Apr 18, 2022 03:40Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema uwezo wa majeshi ya Iran ni uwezo wa kumzuia adui na kuongeza kuwa, uchokozi hata mdogo zaidi wa maadui kama vile utawala wa Kizayuni wa Israel hautafumbiwa macho na vikosi vya ulinzi vya Iran.
-
Iran yalalamika rasmi kuhusu kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu Sweden
Apr 18, 2022 02:42Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imemuita balozi mdogo wa Sweden mjini Tehran na kumfahamisha kuhusu malalamiko makali ya Iran kufuatia kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu na kundi moja lenye misimamo mikali nchini Sweden katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.