-
Sekretarieti ya Kuunga Mkono Intifadha ya Palestian yalaani hatua ya Uingereza dhidi ya HAMAS
Nov 20, 2021 04:45Sekretarieti ya Kudumu ya Mkutano wa Kimataifa wa Kuunga Mkono Intifadha ya Palestina Katika Bunge la Iran imelaani vikali hatua ya serikali ya Uingereza ya kuiweka Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS katika orodha ya makundi ya kigaidi.
-
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran: Sahihi ya rais wa Marekani si ya kutegemewa
Nov 19, 2021 11:50Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema, sharti la kukubaliwa Marekani kurudi kwenye makubaliano ya nyuklia ya JCPOA ni kuondoa Washington kwa namna athirifu, itakayoweza kuthibitika na kwa wakati mmoja vikwazo vyote ilivyoiwekea Iran na kwamba sahihi ya rais wa Marekani haiwezi kutegemewa.
-
"Vikwazo vipya dhidi ya Iran ni muendelezo wa sera zilizofeli za Trump"
Nov 19, 2021 04:22Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu si kitu kingine ghairi ya muendelezo wa sera zilizogonga ukuta za Donald Trump.
-
Lengo la Tehran kushiriki vikao vya Vienna ni kutaka kuondolewa Iran vikwazo vyote haramu
Nov 18, 2021 23:36Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema lengo kuu la Tehran kushiriki mazungumzo ya Vienna kuhusu mapatano ya nyuklia ya JCPOA yanayotazamiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu ni kuhakikisha kuwa taifa la Iran linaondolewa vikwazo vyote haramu.
-
Mchango wa vijana wenye vipaji na viwapa vya juu katika mtazamo wa Kiongozi Muadhamu
Nov 18, 2021 09:58Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu jana Jumatano alihutubia hadhara ya vijana wenye viwapa na vipaji vikubwa vya kieleimu akisisitiza udharura wa jamii ya wasomi kujikita katika suala la kupata njia za kisayansi za kutatua matatizo mbalimbali.
-
Iran: Mafanikio ya mazungumzo ya nyuklia yanategemea iwapo vikwazo vitaendelea
Nov 18, 2021 07:12Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema mafanikio ya mazungumzo ya Iran na kundi la 4+1 yatakayoanza Novemba 29 yatategemea iwapo kutakuwa na irada imara ya upande wa pili ya kuondoa vikwazo au la.
-
Khatibzadeh: Azimio kuhusu hali ya haki za binadamu Iran halina hadhi ya kisheria
Nov 18, 2021 03:51Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema, azimio lililopendekezwa na Canada na kuungwa mkono na baadhi ya nchi za Magharibi kuhusu hali ya haki za binadamu katika Jamhuri ya Kiislamu halina hadhi ya kisheria na kimsingi halikubaliki.
-
Iran: IAEA iache pupa inapozungumzia masuala ya nyuklia
Nov 17, 2021 23:27Kaimu Mwakilishi wa Iran katika taasisi za kimataifa zenye makao yao huko Vienna, Austria ameziasa nchi wanachama wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) zijiepushe kutoa taarifa kwa haraka bila mazingatio juu ya makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.
-
Kiongozi Muadhamu: Matatizo yote ya nchi yanaweza kupatiwa ufumbuzi wa kielimu
Nov 17, 2021 10:21Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, uwezo wa vipawa vya vijana wa taifa la Iran unaweza kuandaa uwanja wa kujaza mapengo ya kielimu ya nchi na ikawezekana kuvuka mipaka ya kimataifa ya kielimu, na hivyo kuleta ustaarabu mpya wa Kiislamu na kuwa na mustakabali unaong’ara.
-
Amir-Abdolahian: Iran na Uturuki ni nchi mbili kubwa katika eneo na mchango wao haupingiki
Nov 16, 2021 23:32Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa ripoti kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram kuhusu mazungumzo yake na waziri mwenzake wa Uturuki hapa Tehran na kusema kuwa, Iran na Uturuki ni nchi mbili kubwa katika eneo la Asia Magharibi na mchango wa nchi hizo mbili katika eneo hilo haukanushiki.