-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq awasili Tehran kwa ziara rasmi ya kikazi
Feb 03, 2021 04:35Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq mapema leo asubuhi amewasili hapa Tehran kwa ajili ya kufanya mazungumzo na viongozi wa ngazi za juu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Iran itatuma sataliti zaidi katika anga za mbali kwa kutumia kombora jipya
Feb 02, 2021 22:59Mkuu wa Kamandi ya Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema nchi hii imeweza kupata mafanikio makubwa baada ya kutuma katika anga za mbali kombora la kisasa kabisa la kubeba satalaiti ambalo linajulikana kama Zuljanah. Amesema kombora la Zuljanah litaweza kutuma satalaiti zaidi katika anga za mbali.
-
Barua ya Iran kwa IAEA: “Sheria ya Hatua za Kistratejia”, uamuzi wa kulinda haki za Iran katika JCPOA
Feb 02, 2021 09:30Mnamo Mei 8 mwaka 2018 Marekani ilichukua hatua ya upande mmoja ya kujitoa katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na kuiwekea tena Iran vikwazo vipya vilivyokuwa vimeondolewa kwa mujibu wa makubaliano hayo, ikitumia sababu mpya na bandia kabisa.
-
Rais Rouhani: Iran itaanza kutoa chanjo ya corona baada ya wiki mbili
Feb 02, 2021 09:13Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema chanjo ya corona au COVID-19 nchini itaanza kutolewa baada ya wiki tatu.
-
Msemaji wa Taliban: Iran inatoa mchango chanya katika mazungumzo ya amani ya Afghanistan
Feb 02, 2021 04:02Msemaji wa ofisi ya kisiasa ya Taliban mjini Doha, Qatar amesema: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inatoa mchango chanya na athirifu katika mchakato wa mazungumzo ya amani ya Afghanistan.
-
Zarif: Marekani sharti itekeleze wajibu wake kwa kurejea katika JCPOA
Feb 02, 2021 00:16Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Marekani haina budi kutekeleza wajibu na majukumu yake kwa kurejea katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.
-
Spika wa Bunge la Iran: Imam Khomeini alihuisha tena Uislamu na heshima ya Waislamu duniani
Feb 01, 2021 08:31Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Imam Khomeini (MA) alihuisha tena Uislamu na izza na heshima ya Waislamu ulimwenguni.
-
Khatibzadeh: Hakutakuweko mazungumzo ya pande mbili baina ya Iran na Marekani
Feb 01, 2021 08:29Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, taifa hili halitafanya mazungumzo na serikali ya Marekani.
-
Mapinduzi ya Kiislamu; miaka 42 ya ukakamavu mkabala na mashinikizo na kuvuka kipindi kigumu
Feb 01, 2021 07:56Miaka 42 iliyopita taifa kubwa la Iran huku likiwa limejizatiti kwa imani thabiti na matumaini ya kuwa na mustkabali mzuri, na bila ya kutegemea dola lolote lenye nguvu duniani, lilifanikiwa kuweka nyuma kipindi kigumu na muhimu kwenye historia yake na hatimaye kufanikiwa kufikia kwa kishindo ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
-
Rais Rouhani: Imam Khomeini MA amewaonesha walimwengu rasilimali ya kijamii
Feb 01, 2021 04:50Rais Hassan Rouhani amesema kuwa, Imam Khomeini MA, mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewaonesha walimwengu rasilimali ya kijamii ya Iran.