-
Iran: Tunafuatilia kwa karibu nyendo za Marekani katika Ghuba ya Uajemi
Jan 04, 2021 12:18Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema Tehran inafuatilia kwa jicho la karibu nyendo na harakati za kutilia shaka za Marekani katika eneo la Ghuba ya Uajemi.
-
Iran yaanza kurutubisha urani kwa asilimia 20 katika kituo cha Fordow
Jan 04, 2021 12:16Msemaji wa serikali ya Iran ametangaza rasmi habari ya kuanza kurutubishwa tena madini ya urani kwa kiwango cha asilimia 20 katika kituo cha nyuklia cha Fordow, kilichoko kaskazini mashariki mwa mji wa Qum kusini mwa mji mkuu wa nchi hii, Tehran.
-
Kukosoa ripota wa Umoja wa Mataifa hatua isiyo ya kisheria ya Marekani ya kumuua Qassim Suleimani
Jan 04, 2021 07:33Januari 3 mwaka uliomalizika hivi majuzi wa 2020, kwa amri ya Rais Donald Trump, utawala wa kigaidi wa Marekani ulifanya jinai ya kumuua kigaidi Luteni Jenerali Qassim Suleimani, Mkuu wa Kikosi cha Quds, cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) na Abu Mahdi al Muhandis, Naibu wa Mkuu wa Harakati ya al Hashd al-Shaabi katika shambulio la anga lililofanywa jirani na uwanja wa ndege wa Baghdad nchini Iraq.
-
Zarif: Mauaji ya Hajj Qassem yanaonesha uchochole wa kupindukia wa Trump
Jan 04, 2021 04:23Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amegusia namna rais wa Marekani Donald Trump alivyotoa amri ya kuuliwa kiwogawoga, shahid Qassem Soleimani, na kusema kuwa, shambulio hilo la anga linaonesha uchochole wa kupindukia wa Donald Trump ambaye ameshindwa kupambana na shujaa huyo katika medani ya mapambano na badala yake alimvizia kiwogawoga uraiani na kumuua.
-
Hijazi: Wanaodhani Israel itawapa amani, wajiulize je Wazayuni hata wameweza kudhamini usalama wao?
Jan 04, 2021 04:21Kaimu Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH amesema kuwa, kuwepo Wazayuni katika eneo hili na hatua ya baadhi ya nchi za Ghuba ya Uajemi za kutangaza uhusiano wa kawaida na Israel ndiko kunakohatarisha usalama na utulivu wa eneo hili.
-
Ali Shamkhani: Chaguo pekee la Marekani ni kuondoa vikwazo vyote dhidi ya Iran
Jan 04, 2021 00:00Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema kuwa, chaguo pekee la Marekani ni kuondoa vikwazo vyote dhidi ya Iran na hivyo kuachana na mkakati wake uliofeli wa mashinikizo ya kiwango cha juu kabisa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Mkuu wa IRIB: Kamanda Suleimani alikuwa dhihirisho la imani, taqwa na kutawakali kwa Allah
Jan 03, 2021 10:15Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB amesema, Luteni Jenerali Qassem Suleimani alikuwa dhihirisho la imani, taqwa na kutawakali kwa Mwenyezi Mungu na alifanya jitihada uhai wake wote katika kushikamana na njia ya fikra ya Imam Khomeini na Ayatullah Khamenei.
-
Brigedia Jenerali Hatami: Iran italipiza kisasi cha kuuawa shahidi Jenerali Suleimani
Jan 03, 2021 04:40Waziri wa Ulinzi wa Iran amesisitiza kuwa, hakuna chembe ya shaka kuwa Jamhuri ya Kiislamu italipiza kisasi cha kuuawa kigaidi Shahidi Luteni Jenerali Qassem Suleimani, aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).
-
Onyo kali la Zarif kwa Trump: Uchezeaji moto wa namna yoyote ile utakabiliwa na jibu kali
Jan 02, 2021 23:24Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ametoa onyo kali kwa rais wa Marekani akisisitiza kuwa; uchezeaji moto wa namna yoyote ile utakabiliwa na jibu kali la Jamhuri ya Kiislamu.
-
Rouhani: Corona imekuwa mtihani wa kihistoria kwa mataifa na viongozi wa dunia
Jan 02, 2021 09:46Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema corona au COVID-19 si ugonjwa wa kawaida bali ni mtihani wa kihistoria kwa mataifa na viongozi wa dunia.