-
Iran yazikosoa nchi za Kiarabu kwa kuzuia taarifa ya NAM ya kulaani vikwazo vya US
Mar 19, 2020 04:23Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa vikali hatua ya baadhi ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote NAM, kwa kuzuia kutolewa taarifa ya jumuiya hiyo ya kulaani vikwazo vya kidhalimu vya Marekani dhidi ya Iran.
-
Bikizee wa miaka 103 apona corona nchini Iran
Mar 18, 2020 09:39Ajuza na bikizee wa miaka 103 aliyekuwa ameambukizwa kirusi cha corona amepona nchini Iran na ameruhusiwa kurudi nyumbani kutoka hospitalini.
-
Shamkhani: Marekani ndiye mtuhumiwa wa kueneza corona, iache kupayuka, itoe majibu kwa walimwengu
Mar 18, 2020 09:36Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema kuwa, upayukaji ndiyo mbinu maarufu inayotumiwa na Marekani ya kukwepa kujibu tuhuma zinazoikabili.
-
Iran yatuma ujumbe kwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Mabunge ya Dunia, yataka kufutwa vikwazo vya dawa vya Marekani
Mar 18, 2020 04:49Katibu Mkuu wa kundi la mabunge la Jumuiya ya Mabunge ya Dunia (IPU) amemtaka Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo kuchukua hatua za kuondoa haraka vikwazo vya dawa, zana na vifaa vya tiba vinavyohitajiwa na wananchi wa Iran kwa ajili ya kupambana na maambukizi ya virusi vya corona.
-
Kuzinduliwa miradi ya kiuchumi na miundo msingi; ishara ya uwezo mkubwa wa Iran
Mar 18, 2020 04:15Tukiwa katika siku za mwisho za mwaka wa Kiirani wa 1398 Hijria Shamshia ambao unamalizika 20 Machi 2020, vyombo vya habari vinajishughulisha kuakisi habari zinazohusu kuenea ugonjwa wa COVID-19 au corona.
-
Takwa la Russia la kuondolewa vikwazo visivyo vya kiutu vya Marekani dhidi ya Iran
Mar 17, 2020 23:39Kuendelea vikwazo vya Marekani vyenye wigo mpana na ambavyo havijawahi kushuhudiwa dhidi ya Iran ambavyo vilianza kutekelezwa baada ya Washington kujiondoa katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA Mei 2018, ni hatua ambayo ilikabiliwa na malalamiko na ukosoaji mkubwa katika uga wa kimataifa ambapo hata washirika wa Ulaya wa Washington nao waliikosoa hatua hiyo isiyo ya kibinadamu.
-
Idara ya Mahakama ya Iran: Vikwazo vya dawa vya Marekani dhidi ya Iran ni kielelezo cha jinai dhidi ya binadamu
Mar 17, 2020 11:34Msemaji wa Idara ya Mahakama nchini Iran amesema kuwa, vikwazo vya kidhalimu vya Marekani kama vikwazo vya dawa na zana za tiba ni kielelezo kikubwa cha utenda jinai wa ubeberu wa kimataifa unaoongozwa na Marekani.
-
Sisitizo la Kamanda Mkuu wa IRGC la utayari wa pande zote wa jeshi hilo kwa ajili ya kukabiliana na corona
Mar 17, 2020 04:36Sambamba na jitihada mtawalia zinazofanywa na kada mbali mbali za utabibu za Wizara ya Afya na Tiba ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran za kukabilianana kirusi cha corona, vikosi vya ulinzi likiwemo Jeshi, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu pamoja na vikosi vya kujitolea vya Basij navyo pia vinashiriki katika harakati hiyo ya kitaifa kwa kutumia kila suhula viliyonayo.
-
IRGC iko tayari kivita kukabiliana na corona nchini Iran
Mar 16, 2020 22:11Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amewapongeza madaktari na wafanyakazi wa sekta ya afya nchini Iran kutokana jihadi yao isiyo na kikomo katika kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19 (corona) na kusema: "Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu liko tayari kivita nchini Iran kukabiliana na kirusi cha corona."
-
Rais Rouhani: Takwimu na kiwango cha mwenendo wa mapambano ya virusi vya Corona, ni zenye kutia matumaini
Mar 16, 2020 08:50Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kupongeza juhudi zisizo na kifani za watumishi wa sekta ya afya nchini hapa katika kupambana na ugonjwa wa Corona, amesema kuwa takwimu na kiwango cha mwenendo wa mapambano dhidi ya virusi vya Corona nchini Iran ni zenye kutia matumaini.