-
Satalaiti ya Zafar yatumwa angani kwa mafanikio licha ya kutofika kwenye mzingo
Feb 10, 2020 00:25Msemaji wa Shirika la Anga za Mbali la Iran (ISA) amesema, satalaiti ya Zafar iliyoundwa na wataalamu wa ndani imerushwa angani kwa mafanikio kwa kutumia roketi la kubebea satalaiti la Simorgh, ijapokuwa haikuweza kufika kwenye mzingo iliopangiwa.
-
Iran yazindua kombora jipya la 'Raad 500'
Feb 09, 2020 08:40Iran imezindua kombora jipya linalojulikana kama 'Raad 500' ambalo linatumia injini aina ya kompositi inayojulikana kama 'Zahir' sambamba na kuzindua kizazi kipya cha makombora ya kijeshi na makombora ya kubeba satalaiti. Uzinduzi huo umehudhuriwa na Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) Meja Jenerali Hussein Salami.
-
Maandamano ya 22 Bahman kufanyika kote Iran katika miji na vijiji 5,200
Feb 09, 2020 08:37Maandamano makubwa ya 22 Bahman (11 Februari) katika kuadhimisha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu yamepangwa kufanyika katika miji na vijiji 5,200 kote Iran.
-
Iran yazima hujuma kubwa ya kiintaneti iliyolenga miundo msingi nchini
Feb 09, 2020 08:28Naibu Waziri wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wa Iran ametangaza kuzumwa hujuma kubwa ya kiintaneti (cyber attack) dhidi ya miundo msingi nchini.
-
Sisitizo la Kiongozi Muadhamu la udharura wa Iran kujiimarisha kinguvu katika pande zote
Feb 09, 2020 08:19Jumamosi ya jana Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na Amiri Jeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi, alikutana na makamanda na watumishi wa kikosi cha anga cha jeshi la Iran ambapo alisisitiza juu ya ulazima wa Iran kuwa na nguvu katika pande zote hususan katika uga wa kiulinzi.
-
Velayati: Muamala wa Karne ni mpango wa kipumbavu; uwepo wa Marekani huko Syria na Iraq umefikia tamati
Feb 09, 2020 04:46Ali Akbar Velayati, Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa amesema kuwa, Muamala wa Karne ni mpango wa kipumbavu kwani Wamarekkani wamefanya biashara na kitu ambacho siyo miliki yao.
-
Uwezo wa Jeshi la Anga la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kujibu vitisho vyovyote na kudumisha usalama katika eneo
Feb 08, 2020 09:41Iran inakaribia kuadhimisha mwaka wa 41 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu. Moja ya fakhari za mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu katika miaka yote hiyo ni kusimama imara mbele ya maadui na kuwa na uwezo wa kujibu kitisho chochote kile dhidi yake.
-
Amiri Jeshi Mkuu: Lazima tuwe na nguvu ili vita visitokee na adui akome kutoa vitisho
Feb 08, 2020 09:28Amiri Jeshi Mkuu wa vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, kuna ulazima wa Iran kuwa na nguvu katika pande zote hasa katika uga wa ulinzi; na akasisitiza kwamba: Ni lazima kuwa na nguvu ili vita visitokee na vitisho vikome.
-
China yaishukuru Iran kwa kutuma misaada ya kitiba kwa ajili ya janga la Corona
Feb 08, 2020 04:37Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China ameishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kutuma misaada ya kitiba kwa ajili ya kukabiliana na virusi vya Corona nchini humo.
-
Shamkhani: Adui atafeli katika vita mahuluti dhidi ya watu wa Iran
Feb 08, 2020 01:10Katibu Mkuu wa Baraza la Uslama wa Taifa la Iran amesema kukuza mambo kupita kiasi na vitisho ni mbinu inayotumiwa na adui katika vita vya kipropaganda dhidi ya watu wa Iran na kusema bila shaka Wazayuni, Wamagharibi na vibaraka wao katika nchi za Kiarabu watafeli katika njama hiyo.