Shamkhani: Adui atafeli katika vita mahuluti dhidi ya watu wa Iran
Katibu Mkuu wa Baraza la Uslama wa Taifa la Iran amesema kukuza mambo kupita kiasi na vitisho ni mbinu inayotumiwa na adui katika vita vya kipropaganda dhidi ya watu wa Iran na kusema bila shaka Wazayuni, Wamagharibi na vibaraka wao katika nchi za Kiarabu watafeli katika njama hiyo.
Admeli Ali Shamkhani, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran ameyasema hayo Ijumaa mjini Tehran ambapo amefafanua kuhusu njama kadhaa ambazo Marekani inaendelea kutekeleza dhidi ya Iran na kusema: "vita mahuluti vya Marekani vinatekelezwa kwa lengo la kuilazimu Iran isalimu amri na kusambaratisha mfumo wa Kiislamu lakini njama hiyo itafeli kutokana na elimu, ufahamu, uwajibikaji, kuwa macho, utayarifu na mshikamano wa watu wa Iran."
Shamkhani ameongeza kuwa, dikteta Saddam aliyepinduliwa Iraq, akiwa na waitifaki wake, walikuwa na dhana kuwa vikosi vya ulinzi vya Iran havikuwa tayari na hivyo wakailzaimisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuingia vitani; lakini umoja wa watu wa Iran na utayarifu wa vikosi vya ulinzi vya Iran ni nukta mbili ambazo zilithibitisha kuwa hatima ya wenye dhana potovu ni kushindwa na mauti.

Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema watu wa Iran kwa kutegemea ustaarabu mkongwe, dini, mapinduzi na kutumia uwezo wao mkubwa wataweza kukabiliana na vitisho vya zama hizi na kuibuka washindi na hivyo kuendelea kwa nguvu na uwezo katika mkondo wa ustawi wa mfumo wa Kiislamu.