-
Baghaei: Wafuasi wa utawala katili wa Israel lazima waache kushiriki mauaji ya kimbari
Sep 19, 2025 00:57Ismail Baghaei, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumzia ripoti ya hivi karibuni ya Umoja wa Mataifa na kusema kuwa, ripoti ya Tume ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa haikubakisha chembe ya shaka kwamba jinai za Israel huko Ghaza ni mauaji ya kimbari, hivyo waungaji mkono wa utawala huo ghasibu wanapaswa kuacha kushiriki katika mauaji ya kimbari ya Wapalestina.
-
Saudia yaitaarifu rasmi Iran makubaliano yake ya kijeshi na Pakistan
Sep 18, 2025 23:08Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia amefanya mazungumzo ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje ya Iran n kumtaarifu rasmi kuhusu makubaliano ya hivi karibuni ya ulinzi ya Saudia na Pakistan.
-
Ushirikiano wa Iran na Saudi Arabia kwenye njia ya kusaidiana na utaratibu mpya wa kikanda
Sep 18, 2025 07:41Ali Larijani, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Mohammed bin Salman, Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudi Arabia wamekutana mjini Riyadh na kujadili uhusiano wa pande mbili na matukio ya kieneo.
-
Pezeshkian: Ushirikiano wa "mafanikio" wa Iran na Russia unaashiria mwisho wa zama za uchukuaji hatua za upande mmoja
Sep 18, 2025 07:34Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kigezo "kilichofanikiwa" cha ushirikiano kati ya nchi huru, zikiwemo na Iran na Russia, utathibitisha kwamba zama za uchukuaji hatua za upande mmoja duniani zimemalizika.
-
Araqchi: Nchi za Ulaya zinapasa kuonyesha nia ya dhati na ya kweli katika diplomasia
Sep 18, 2025 03:54Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araqchi jana amezungumza kwa simu na Mawaziri wenzake wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Ujerumani na Uingereza na pia na mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Umoja wa Ulaya kujadili kadhia ya nyuklia na kuondoa vikwazo haramu na kusema: Wakati umefika sasa kwa nchi za Ulaya kudhihirisha nia ya dhati na ya kweli katika diplomasia.
-
Eslami: Vitisho vya maadui vinaendelea; hali ya kuaminiana na IAEA inapasa kujengwa upya
Sep 18, 2025 03:54Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran amesema vitisho kutoka kwa maadui wa Jamhuri ya Kiislamu vinaendelea tangu kujiri mashambulizi ya Israel na Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya nchi hii.
-
Iran yayataja kuwa ya kipuuzi madai ya Marekani kuhusu mpango wake wa makombora
Sep 18, 2025 01:10Iran imetaja kuwa ya kipuuzi madai ya Marekani kuhusu ustawi wake katika sekta ya makombora, ikielezea mpango huo kuwa wa kujihami dhidi ya mashambulizi ya Marekani na Israel.
-
Jenerali: Uwezo wa Iran wa kivita unawazuia maadui kuanzisha mashambulizi mapya
Sep 18, 2025 02:35Mkuu wa Majeshi ya Iran, Meja Jenerali Abdolrahim Mousavi, amepongeza kuimarika kwa uwezo wa kujihami wa taifa , akisisitiza kuwa utayari wa Iran wa kivita umezuia maadui kuanzisha duru mpya ya mashambulizi dhidi ya nchi.
-
Kiongozi wa Mapinduzi aipongeza timu ya miereka kwa kutwaa ubingwa wa dunia
Sep 17, 2025 10:21Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ameipongeza timu ya taifa ya Iran ya mchezo wa miereka ya freestyle kwa kutwaa taji la ubingwa wa dunia katika Mashindano ya Miereka ya Dunia ya 2025 yaliyofanyika mjini Zagreb, Croatia.
-
Iran yatekeleza hukumu ya kifo dhidi ya jasusi wa Mossad ya Israel katika Vita ya Siku 12
Sep 17, 2025 08:55Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetekeleza hukumu ya kifo dhidi ya Babak Shahbazi, raia aliyekutwa na hatia ya kushirikiana na shirika la kijasusi la utawala wa Israel, Mossad, kwa kutoa taarifa nyeti kuhusu maeneo ya kiusalama ya Iran wakati wa vita ya siku 12 vya kichokozi vya utawala huo mwezi Juni.