-
UN katika mzingiro wa ukwamishaji wa Marekani; Washington yakataa kumpa viza Zarif
Jan 11, 2020 08:03Majid Takhte Ravanchi, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amemuandikia barua Katibu Mkuu wa umoja huo na kubainisha malalamiko makali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ukwamishaji wa serikali ya Trump wa kutompa viza Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran kwa ajili ya kushiriki katika kikao cha Baraza la Usalama.
-
Rais Rouhani: Kosa la kibinadamu kutokana na vitisho vya Marekani ndiyo sababu ya kuanguka ndege ya Ukraine
Jan 11, 2020 04:40Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kosa la kibinadamu lililotokana na vitisho vya Marekani vya kushambulia maeneo nyeti nchini Iran ndiyo sababu ya kuanguka ndege ya abiria ya Ukraine karibu na Tehran.
-
Ulaya yapinga ombi la Trump la kujiondoa JCPOA
Jan 11, 2020 01:21Umoja wa Ulaya sambamba na nchi tatu za Ulaya za Ufaransa, Ujerumani na Uingereza zinazojulikana kama Troika ya Ulaya, ni waungaji mkono wa mapatano ya kimataifa ya nyuklia maarufu kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji JCPOA.
-
Scott Ritter: Trump amelegeza msimamo kwa kuogopa jibu kali la Iran
Jan 11, 2020 01:21Scott Ritter, aliyewahi kuwa mkaguzi wa silaha wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, Rais Donald Trump wa Marekani amelegeza msimamo na kuachana na vitisho vyake alivyovitoa hapo kabla dhidi ya Iran kutokana na kuhofia jibu kali la Tehran.
-
Hatibu wa sala ya Ijumaa Tehran: Qassem Soleimani alikuwa mratibu wa usalama
Jan 10, 2020 08:44Hatibu wa sala ya Ijumaa mjini Tehran amemtaja shahidi Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran kuwa ni mratibu wa usalama na amani.
-
Rais Rouhani wa Iran: Wamarekani wahitimishe hatua zao ghalati
Jan 10, 2020 08:33Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa anataraji kwamba Wamarekani watahitimisha hatua zao ghalati, lakini iwapo watatekeleza hatua nyingine iliyo dhidi ya maslahi ya Iran, basi watapata jibu kali mkabala.
-
Mashauriano ya kidiplomasia ya Iran kwa ajili ya kuarifisha jinai za Marekani
Jan 10, 2020 07:30Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika mazungumzo yake ya simu na viongozi wa nchi kadhaa jirani, nchi za Ulaya na Afrika kwamba Iran inaunga mkono amani na usalama lakini haitakaa kimya mbele ya vitimbi vya Marekani.
-
Iran yajibu uvumi unaoenezwa kuhusu chanzo cha ajali ya ndege ya Ukraine
Jan 10, 2020 00:20Mkuu wa shirika la ndege la Iran amesema: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ndio yenye wajibu wa kuchunguza ajali ya ndege ya abiria aina ya Boing 737 ya Ukraine iliyoanguka katika anga ya mji wa Tehran.
-
Kamanda Hajizadeh: Operesheni ya SEPAH ni mwanzo wa mchakato wa kutoka wanajeshi wa Marekani Asia Magharibi
Jan 09, 2020 21:06Kamanda wa Kikosi cha Anga za Mbali cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH amezungumzia mashambulizi ya makombora yaliyofanywa na jeshi hilo kwenye kambi za wanajeshi magaidi wa Marekani nchini Iraq na kuongeza kuwa, thamani ya damu ya shahid Luteni Jenerali Qassem Soleimani ni kufukuzwa kikamilifu wanajeshi wa Marekani katika eneo hili, na shambulio hilo la SEPAH ndio mwanzo wa mchakato huo.
-
Rais Rouhani: Umoja wa Ulaya unapaswa kuwa na misimamo huru, usiburuzwe na Marekani
Jan 09, 2020 21:06Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, mahesabu ghalati na yenye madhara makubwa ya Marekani yanatokana na kushindwa nchi hiyo kuielewa vizuri Iran na eneo la Asia Magharibi. Amesisitiza kuwa, Umoja wa Ulaya unapaswa kuwa huru na usikubali kuburuzwa na Marekani na kuifanya Iran ikate tamaa kikamilifu na umoja huo.