-
Iran yajibu uvumi unaoenezwa kuhusu chanzo cha ajali ya ndege ya Ukraine
Jan 10, 2020 00:20Mkuu wa shirika la ndege la Iran amesema: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ndio yenye wajibu wa kuchunguza ajali ya ndege ya abiria aina ya Boing 737 ya Ukraine iliyoanguka katika anga ya mji wa Tehran.
-
Kamanda Hajizadeh: Operesheni ya SEPAH ni mwanzo wa mchakato wa kutoka wanajeshi wa Marekani Asia Magharibi
Jan 09, 2020 21:06Kamanda wa Kikosi cha Anga za Mbali cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH amezungumzia mashambulizi ya makombora yaliyofanywa na jeshi hilo kwenye kambi za wanajeshi magaidi wa Marekani nchini Iraq na kuongeza kuwa, thamani ya damu ya shahid Luteni Jenerali Qassem Soleimani ni kufukuzwa kikamilifu wanajeshi wa Marekani katika eneo hili, na shambulio hilo la SEPAH ndio mwanzo wa mchakato huo.
-
Rais Rouhani: Umoja wa Ulaya unapaswa kuwa na misimamo huru, usiburuzwe na Marekani
Jan 09, 2020 21:06Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, mahesabu ghalati na yenye madhara makubwa ya Marekani yanatokana na kushindwa nchi hiyo kuielewa vizuri Iran na eneo la Asia Magharibi. Amesisitiza kuwa, Umoja wa Ulaya unapaswa kuwa huru na usikubali kuburuzwa na Marekani na kuifanya Iran ikate tamaa kikamilifu na umoja huo.
-
Mwamko wa walimwengu na kuchanganyikiwa NATO na Marekani kuhusu Luteni Soleimani
Jan 09, 2020 21:02Radiamali na hisia zilizooneshwa na baadh iya viongozi wa nchi za Magharibi baada ya Marekani kumuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH kwa mara nyingine zimeonesha undumilakuwili wa viongozi wa nchi za Magharibi kuhusu madai yao ya kupambana na magaidi.
-
Rouhani amwambia Johnson: Kama si Jenerali Soleimani hii leo London isingekuwa na amani
Jan 09, 2020 10:03Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameitaka serikali ya Uingereza ibadili msimamo wake kuhusiana na mauaji ya kigaidi yaliyofanywa na Marekani dhidi ya Jenerali Qassem Soleimani.
-
Kiongozi Muadhamu ashiriki marasimu ya kumbukumbu ya kuuliwa shahidi Luteni Jenerali Soleimani na wanamapambano wenzake
Jan 09, 2020 08:31Marasimu ya kumbukumbu ya kuuliwa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani na wanajihadi wenzake yamefanyika leo hapa Tehran katika Husseiniya ya Imam Khomeini kwa kuhudhuriwa na Kingozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Khamenei.
-
Marekani: Tuko tayari kufanya mazungumzo na Iran bila masharti
Jan 09, 2020 02:38Serikali ya Marekani imetangaza kuwa, iko tayari kufanya mazungumzo na Iran bila masharti yoyote.
-
Kiongozi Muadhamu atoa mkono wa pole kufuatia vifo vya waliofariki mazikoni Kerman na katika ajali ya ndege Tehran
Jan 08, 2020 21:49Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa ujumbe maalumu wa mkono wa pole kufuatia kufariki dunia wananchi kadhaa wakati wa kusindikiza jeneza la mwili mtoharifu wa shahidi Kamanda Qassem Soleimani wakati wa maziko yake yaliyofanyika mkoani Kerman na vile vile wananchi walioaga dunia katika tukio la ajali ya ndege ya abiria iliyoanguka hapa mjini Tehran.
-
Iran: Tuliipa taarifa serikali ya Iraq kuhusu operesheni ya makombora dhidi ya kituo cha kijeshi cha Marekani
Jan 08, 2020 21:47Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema, Jamhuri ya Kiislamu iliipa taarifa serikali ya Iraq kuhusu operesheni ya makombora iliyofanywa na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu dhidi ya kambi ya kijeshi ya Marekani ya Ainul-Assad na kusisitiza kuwa: Tehran inaheshimu na kuthamini mno kujitawala na umoja wa ardhi yote ya Iraq.
-
Sisitizo la Kiongozi Muadhamu la udharura wa kuhitimishwa uwepo haribifu wa Marekani Asia Magharibi
Jan 08, 2020 10:29Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu asubuhi ya leo amekutana hapa mjini Tehran na maelfu ya wananchi kutoka mji wa Qum kwa mnasaba wa kukaribia kumbukumbu ya Harakati ya Kihistoria ya Dei 19 iliyosadifiana na Januari 1978 ambapo sanjari na kubainisha kubainisha sifa maalumu za kishakhsia za Luteni Jenerali Qassim Soleimani ametoa tathmini jumla kuhusiana na matukio ya eneo na ustawi wa Mapinduzi ya Kiislamu.