-
Mamilioni ya Wairani wauaga mwili wa Jenerali Qassem Soleimani na mashahidi wenzake
Jan 06, 2020 09:52Marasimu ya kuuaga mwili wa shahidi Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC, yamefanyika kwa kuhudhuriwa na mamilioni ya watu mjini Tehran.
-
Kiongozi Muadhamu asalisha Sala ya Maiti ya Luteni Jenerali Soleimani na mashahidi wenzake + Video
Jan 06, 2020 04:46Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo asubuhi amesalisha Sala ya Maiti ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH na mashahidi wenzake waliouliwa kigaidi na Marekani nchini Iraq, usiku wa kuamkia Ijumaa ya tarehe 3 Januari 2020.
-
Rouhani: Inabidi tusimame imara katika kukabiliana na uingiliaji wa Marekani
Jan 06, 2020 04:45Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, usiku wa kuamkia leo amefanya mazungumzo ya simu na Rais Barham Salih wa Iraq na kusisitiza kuwa, ni jambo zito mno kwa mataifa makubwa ya Iran na Iraq kuweza kuvumilia mauaji ya kigaidi waliyofanyiwa Alhaj Qassem Soleimani, Abu Mahdi al Muhandis na wanamapambano wenzao waliokuwa wamefuatana nao.
-
Iran: Marekani ikitushambulia tutaingamiza Israel na kuifuta katika uso wa dunia
Jan 06, 2020 04:44Katibu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika maombolezo ya kukumbuka kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani; Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH kwamba, iwapo Marekani itatekeleza vitisho vinavyotolewa na Trump vya kuishambulia Iran, basi wawe na yakini kwamba miji ya Haifa na Tel Aviv na maeneo mengine muhimu ya Israel yataangamizwa kikamilifu na kusawazisha na ardhi.
-
Ismail Hania ametoka Ghaza kuja Tehran kushiriki maziko ya Kamanda Soleimani; asema Soleimani ni shahidi wa Quds + Video
Jan 06, 2020 04:43Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ametilia mkazo wajibu wa kuendelea na muqawama hadi ardhi zote za Palestina zitakapokombolewa.
-
Iran yasitisha utekelezaji wa makubaliano ya JCPOA
Jan 06, 2020 00:08Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran usiku wa kuamkia leo Jumatatu imetoa taarifa ikitangaza kuwa imechukua hatua ya tano na ya mwisho ya kupunguza utekelezaji wa ahadi zake katika makubaliano ya nyuklia maarufu kwa kifupi kama JCPOA.
-
Zarif: Tishio la Trump dhidi ya maeneo ya kiutamaduni ya Iran ni jinai ya kivita
Jan 05, 2020 23:17Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amejibu tishio alilotoa Ras wa Marekani dhidi ya wananchi wa Iran kupitia ukurasa wake wa Twitter na kusisitiza kuwa: Tishio hilo dhidi ya maeneo ya kiutamaduni ni jinai ya kivita.
-
Kiongozi wa Russia: Jenerali Qassem Soleimani alikuwa shujaa wa ulimwengu wote wa Kiislamu
Jan 05, 2020 23:15Mkuu wa Taasisi ya Kimataifa inayoitwa 'Umma Mmoja wa Kiislamu' nchini Russia amesema kuwa, Meja Jenerali Qassem Soleimani, hakuwa tu mtu wa Iran, Iraq au Syria, bali ni shakhsia wa Kiislamu na ulimwengu kwa ujumla.
-
Waziri wa Ulinzi wa Iran; Ulimwengu mzima una wajibu wa kukabiliana na hatua ya kigaidi ya Marekani
Jan 05, 2020 23:10Waziri wa Ulinzi wa Iran amesema kuwa ulimwengu mzima una wajibu wa kukabiliana na hatua ya kigaidi ya Marekani ya kumuua shahidi Kamanda Qassem Soleimani; na watu wote wanapaswa kutekeleza majukumu yao mbele ya jinai hiyo.
-
Mwili wa shahidi Qassem Soleimani na ya mashahidi wenzake yasindikizwa na kuagwa Ahvaz na Mashhad + Video
Jan 05, 2020 12:10Mwili wa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, kamanda wa kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu na ya mashahidi wenzake waliouliwa shahidi pamoja naye katika jinai ya kinyama iliyofanywa na majeshi ya kigaidi ya Marekani imesindikizwa na kuagwa leo katika mji mtakatifu wa Mashhad kaskazini mwa Iran na huko Ahvaz kusini mwa nchi.