-
Zarif: Iran haitoanzisha vita vya aina yoyote
Sep 24, 2019 09:43Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kubainisha kwamba Iran haitoanzisha vita vyovyote, amesema kuwa, iwapo Tehran itashambuliwa, basi itajitetea kwa uwezo wake wote.
-
Azimio la haki za binadamu la Ulaya dhidi ya Iran na sera za kindumakuwili kuhusu haki za binadamu
Sep 24, 2019 04:02"Suala la kulinda na kuheshimu haki za binadamu ni miongoni mwa mambo ya wajibu kisheria na kikanuni nchini Iran na wala utekelezaji wake hapa nchini hauhitajii matamshi ya kichochezi ya nchi nyingine."
-
Rouhani: Madai ya Ujerumani, Uingereza na Ufaransa dhidi Iran hayana msingi wowote
Sep 24, 2019 00:19Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa vikali tuhuma zilizotolewa na Ujerumani, Uingereza na Ufaransa kuwa eti Iran ilihusika katika mashambulizi yaliyolenga kituo kikubwa cha kusafisha mafuta cha Aramco nchini Saudi Arabia na kusisitiza kuwa, madai hayo haya msingi wowote.
-
Safari ya Rais Rouhani New York: Matarajio kutoka kikao cha 74 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
Sep 23, 2019 09:41Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu leo Jumatatu ameelekea mjini New York Marekani kwa ajili ya kushiriki kikao cha 74 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kilichoanza leo Jumatatu. Katika safari yake hiyo, Rais Rouhani atatoa hotuba mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kama ambavyo ataonana pia na viongozi mbalimbali wa nchi wanaoshiriki katika kikao hicho.
-
Rouhani: Kutengwa hivi sasa Marekani hakujawahi kushuhudiwa katika historia ya uhasama na Iran
Sep 23, 2019 09:09Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekutaja kutengwa hivi sasa Marekani kuwa hakujawahi kushuhudiwa katika historia ya uhasama na Iran.
-
Msemaji wa serikali ya Iran: Marekani imeyateka makao makuu ya Umoja wa Mataifa
Sep 23, 2019 08:54Msemaji wa serikali ya Iran amesema kuwa Marekani imeyateka makao makuu ya Umoja wa Mataifa. Ameyasema hayo katika radiamali kwa hatua ya Marekani ya kuweka vizuizi katika kutoa viza kwa ujumbe wa kidiplomasia wa Iran kwa ajili ya kushiriki katika kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
-
Rais Rouhani: Maneno ya haki yanayobainishwa na Iran ni machungu mno kwa Marekani
Sep 23, 2019 04:41Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kabla ya kuondoka Tehran kuelekea New York kwa ajili ya kushiriki katika kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwamba, ataitumia safari hiyo kubainisha maneno ya haki ya taifa hili ambayo ni machungu kwa Marekani.
-
Zarif: Wayemen wamelenga kiwanda cha kusafirisha mafuta Saudia na si hospitali wala shule
Sep 22, 2019 23:54Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa msimamo wa Marekani kuhusiana na mashambulizi yaliyofanywa na wapiganaji wa harakati ya Ansarullah nchini Yemen dhidi ya taasisi za mafuta za Saudi Arabia na kusisitiza kuwa, Wayemeni wamefanya mashambulizi hayo ya ndege zisizo na rubani kulipiza kisasi cha mashambulizi ya zaidi ya miaka mine sasa ya Riyadh ambayo yameua mauaji ya mamia ya maelfu ya raia wasio na hatia.
-
Rais Rouhani: Kuweko mifarakano katika eneo, ndilo takwa la Marekani na Uzayuni
Sep 22, 2019 09:27Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kuweko mifarakano baina ya mataifa ya Mashariki ya Kati ndilo takwa la Marekani na Uzayuni.
-
Dakta Zarif: Vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran vinafunga milango yote ya mazungumzo
Sep 22, 2019 09:25Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambaye ameelekea New York Marekani kwa ajili ya kushiriki katika mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa amekosoa vikali hatua mpya ya Marekani dhidi ya Iran.