-
Waumini 80,000 wa Kipalestina washiriki Swala za Ijumaa katika Msikiti wa Al-Aqsa
Mar 15, 2025 08:58Waumini wapatao 80,000 wa Kipalestina walishiriki swala ya Ijumaa ya pili ya mwezi mtukufu wa Ramadhani katika Msikiti wa Al-Aqsa jijini Al Quds (Jerusalem) licha ya vizuizi vikali vilivyowekwa na Israel kuwazuia Waislamu kufika katika eneo hilo takatifu.
-
Associated: Marekani na Israel zilitaka kuwapa makazi wakazi wa Gaza katika nchi tatu za Kiafrika
Mar 14, 2025 22:55Shirika la habari la Associated Press limeripoti kuwa Marekani na Israel zilitoa pendekezo kwa maafisa wa nchi tatu za Afrika la kuwapa makazi Wapalestina kutoka Ukanda wa Gaza kwenye ardhi za nchi hizo.
-
Mustakbali uliogubikwa na kiza wa Syria; wafuasi wa al Julani wazidi kuua raia
Mar 14, 2025 04:45Shirika la kutetea haki za binadamu nchini Syria limeripoti habari ya kuuawa zaidi ya raia 1,383 wasio na hatia katika shambulio lililofanywa na magenge yenye mfungamano na watawala wa hivi sasa wa Syria kwenye maeneo ya Waislamu wa Kishia, magharibi mwa nchi hiyo ya Kiarabu.
-
Ndege za Israel zashambulia viunga vya Damascus na kusonga mbele Quneitra
Mar 14, 2025 03:22Israel imefanya shambulizi la anga katika viunga vya Damascus huku vifaru vyake vikiendelea kusonga ndani zaidi ya eneo la kusini-magharibi la Quneitra, ikiwa ni sehemu ya uchokozi wake wa hivi karibuni dhidi ya Syria tangu kuondolewa kwa Rais Bashar al-Assad.
-
Taarifa ya UN: Israel imetenda Mauaji ya Kimbari Gaza
Mar 14, 2025 03:22Ripoti maalum ya Tume Huru ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa imebaini kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel umetekeleza mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza kwa kuharibu kwa makusudi vituo vya huduma za afya ya uzazi wakati wa mashambulizi yake makali katika eneo hilo.
-
Yedioth Ahronoth: Kipindi cha fungate ya Trump na Netanyahu kimekwisha
Mar 13, 2025 06:58Gazeti la Kizayuni la Yedioth Ahronoth limeandika katika makala kwamba baraza la mawaziri la utawala huo linaloongozwa na Netanyahu limekuwa chini kabisa ya ajenda ya Marekani.
-
Hamas: Oparesheni ya Salfit ni ujumbe wa muqawama katika kujibu chokochoko za adui
Mar 13, 2025 04:03Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imesisitiza katika taarifa kuwa oparesheni ya ufyatuaji risasi iliyotekelezwa jana usiku karibu na eneo la Salfit katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan ni jibu jipya la watu wao na wanamuqawama huru wa Palestina katika kujibu mashambulizi ya kikatili ya utawala ghasibu wa Israel khususan kaskazini mwa ukingo huo.
-
Hamas: Duru mpya ya mazungumzo ya kusitisha mapigano imeanza
Mar 12, 2025 22:52Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ameeleza kuwa duru mpya ya mazungumzo ya kusimamisha vita Ukanda wa Gaza, imeanza.
-
Hamas yasema hatua ya Israel kuzuia misaada kuingia Gaza ni ‘Uhalifu wa Kivita’
Mar 12, 2025 09:11Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, imesema kuwa uamuzi wa utawala haramu wa Israel wa kuzuia kuingia kwa misaada ya kibinadamu na mahitaji ya msingi katika Ukanda wa Gaza unaozingirwa ni "uhalifu wa kivita."
-
Yemen yaanza tena kushambulia meli za Israel baada ya kukataa kufungua vivuko vya Ghaza
Mar 11, 2025 23:42Yemen imetangaza kuanza tena operesheni za kijeshi za kushambulia meli za Israel katika maeneo muhimu ya baharini karibu na fukwe zake kufuatia kumalizika muda wa mwisho ilioupa utawala wa Kizayuni wa kufungua tena vivuko vya Ukanda wa Ghaza na kuruhusu misaada kuwafikia Wapalestina iliowasababishia hasara kubwa kutokana na mashamblizi yake ya kikatili ya zaidi ya miezi 15.