-
Ripota Maalumu wa UN afichua nafasi ya Ujerumani na Marekani katika mauaji ya kimbari ya Israel huko Gaza
Dec 28, 2024 04:01Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa Kuhusu Haki za Binadamu na Kupambana na Ugaidi amesema: Marekani na Ujerumani zinadhamini asilimia 99 ya silaha za utawala wa Kizayuni wa Israel na inawezekana kuchukuliwa hatua za kisheria dhidi ya nchi hizo.
-
Mamilioni ya Wayemeni walaani jinai za Wazayuni dhidi ya taasisi za kiraia
Dec 27, 2024 23:37Mamilioni ya wananchi wa Yemen walimiminika mabarabarani jana Ijumaa huko Sana'a na mikoa mingine, kulaani hujuma na jinai za Wazayuni wanaoshambulia maeneo na taasisi za kiraia katika mji mkuu, Sana'a na mkoani Hudaydah.
-
Umaskini washadidi Israel, milioni mbili wanaishi chini ya mstari wa umaskini
Dec 27, 2024 23:18Vita vinaweza kuwa biashara nzuri kwa watengenezaji silaha, lakini, kwa upande wa Israel, ni habari mbaya kwa idadi ya watu. Umaskini umezikumba ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu ambazo zimepachikwa jina bandia la Isarel. Waziri mkuu wa Israe Benjamin Netanyahu ameingia katika vita ambavyo vimewatumbukiza Wazayuni katika masaibu makubwa.
-
Jinai za Israel zinaendelea: Wapalestina wengine 15 wauawa shahidi
Dec 27, 2024 07:38Wapalestina wengine 15 wameuawa shahidi katika jinai ya hivi punde ya jeshi la utawala wa Kizayuni katika ukanda wa Gaza.
-
Kiongozi wa Ansarallah: Marekani na Israel zinafuatilia kuugawa Ulimwengu wa Kiislamu
Dec 27, 2024 07:18Kiongozi wa Ansarallah wa Yemen, Abdul Malik al-Houthi, amesema kuwa, Marekani na 'Israel' zinafanya njama za kuudhibiti ulimwengu wa Kiislamu kwa njia ya mgawanyiko na ukandamizaji, akisisitiza umuhimu wa kuendelezwa muqawama na mapambano.
-
New York Times: Jeshi la Israel liliidhinisha kuuliwa raia mpaka 100 Ghaza ili kumpata mshukiwa mmoja wa Hamas
Dec 27, 2024 04:13Uchunguzi uliofanywa na gazeti la New York Times la Marekani unaonyesha kuwa, jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel lililegeza kwa kiwango kikubwa sheria zake za kivita katika miezi ya mwanzo ya vita vyake dhidi ya Ghaza, na kusababisha vifo vingi vya raia.
-
Iraq yafukua mabaki ya miili 100 ya Wakurdi wanawake na watoto waliouliwa na Saddam
Dec 27, 2024 03:55Mamlaka ya Iraq imeanza kufukua mabaki ya miili ya wanawake na watoto wapatao 100 wa Kikurdi walioripotiwa kuuliwa na utawala wa Saddam Hussein katika miaka ya 1980.
-
Licha ya hujuma za kinyama za Israel Sana'a na Hudaydah, kombora jengine la Yemen lapiga Tel Aviv
Dec 27, 2024 00:08Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni vimeripoti kuwa ving'ora vya tahadhari ya mashambulio ya anga vimesikika katika sehemu kubwa ya maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu yaliyopachikwa jina bandia la Israel kufuatia shambulio la kombora lililorushwa kutoka Yemen mapema leo.
-
Hamaki ya Tel Aviv dhidi ya matamshi ya Papa kuhusu jinai za utawala wa Kizayuni
Dec 26, 2024 10:08Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya utawala wa Kizayuni wa Israel imemwita balozi wa Vatican katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu kwa ajili ya kusailiwa. Ni baada ya Papa Francis, kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani kukosoa vita na mauaji ya Israel katika Ukanda wa Gaza.
-
'Kristo bado yuko chini ya vifusi vya Gaza', kasisi wa Palestina asema katika ujumbe wa Krismasi
Dec 26, 2024 08:41"Kristo bado yuko chini ya vifusi vya Gaza huku eneo la Palestina lililozingirwa likiangamizwa". Haya yamesemwa na Munther Isaac, mchungaji na mwanatheolojia maarufu wa Kikristo wa Palestina, katika ujumbe wake wa kila mwaka wa Sikukuu ya Krismasi.