Umaskini washadidi Israel, milioni mbili wanaishi chini ya mstari wa umaskini
Vita vinaweza kuwa biashara nzuri kwa watengenezaji silaha, lakini, kwa upande wa Israel, ni habari mbaya kwa idadi ya watu. Umaskini umezikumba ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu ambazo zimepachikwa jina bandia la Isarel. Waziri mkuu wa Israe Benjamin Netanyahu ameingia katika vita ambavyo vimewatumbukiza Wazayuni katika masaibu makubwa.
Kwa mujibu wa ripoti ya hivi karibuni ya Taasisi ya Kitaifa ya Bima, karibu Waisraeli milioni 2, yaani 20% ya idadi ya watu katika utawala wa Kizayuni, wanaishi chini ya mstari wa umaskini.
Vijana walio chini ya miaka 29 wameathirika zaidi, huku 47.2% wakiishi chini ya mstari wa umaskini.
Hali ni mbaya haswa kwa familia zenye watoto kwani watoto 872,000, ambao ni 9% ya watoto wote Israel, wanaishi katika umaskini.
Mkusanyiko mkubwa zaidi wa umaskini unaweza kupatikana katika eneo la Al Quds (Jerusalem), ambapo 48.3% ya familia zimeainishwa kama maskini, zikifuatiwa na mikoa ya kaskazini na kusini, yenye kiwango cha umaskini cha 22.5% na 22.6% mtawalia.
Ingawa Israeli tayari ilikuwa inateseka kiuchumi kabla ya Oktoba 7, 2023, sasa imekumbwa na mzozo wa kiuchumi kutokana na vita vilivyoanzishwa na utawala wa Netanyahu.
Sasa Israel inakabiliwa na tishio lililopo kutoka kwa deni la karibu dola bilioni 336, hadi Pato la Taifa linaloporomoka. Pato la Taifa lilishuka kutoka 6.5% mnamo 2022 hadi karibu 2% mnamo 2023 na mwaka 2024 pato hilo limefika sifuri. Hivyo hakuna shaka kuwa kutashuhudiwa kuporomoka uchumi na jamii ya