-
Kiongozi wa Tahrir al-Sham: Hatutaruhusu Syria itumike kufanyia mashambulio dhidi ya Israel
Dec 17, 2024 02:35Kiongozi wa kundi la wanamgambo wa Hay'at Tahrir al-Sham (HTS), ambalo liliiondoa madarakani serikali ya Syria mapema mwezi huu huku kukiwa na taarifa zilizoenea za kuungwa mkono kundi hilo na mataifa ya Magharibi na Israel, amesema hataruhusu ardhi ya Syria itumike kufanyia mashambulizi dhidi ya Israel.
-
Jeshi la Kizayuni lamuua Babu mtu wa Kipalestina aliyegusa nyoyo za walimwengu mitandaoni
Dec 17, 2024 02:35Shambulio la kinyama la makombora lililofanywa na jeshi la Kizayauni katika Ukanda wa Ghaza limemuua Khaled Nabhan, Mpalestina ambaye amefahamika sana kwenye mitandao ya kijamii kutokana na video iliyomuonyesha akibusu macho ya mjukuu wake aliyeuliwa na kumwita "roho ya roho yangu".
-
Harakati ya Ukombozi ya Wananchi wa Palestina: Mashambulizi ya Mamlaka ya Ndani dhidi ya Muqawama ni kuvuka mstari mwekundu
Dec 16, 2024 23:56Harakati ya Wananchi kwa ajili ya Ukombozi wa Palestina (PFLP) imetangaza kuwa mashambulizi ya vikosi vya Mamlaka ya Ndani ya Palestina dhidi ya wanamapambano wa Kipalestina katika mji wa Jenin ni kuvuka mstari mwekundu.
-
Nchi za Kiarabu zalaani mpango wa Israel wa kujenga vitongoji katika ardhi ya Syria
Dec 16, 2024 23:25Nchi kadhaa za Kiarabu zimelaani mradi mpya wenye utata wa utawala haramu wa Israel wa kupanua vitongoji vyake haramu vya walowezi katika Miinuko ya Golan inayokaliwa kwa mabavu, zikieleza uungaji mkono wao kwa kulindwa mamlaka ya kujitawala Syria katika eneo hilo la milima.
-
Israel yafanya mashambulizi mengine makubwa ya anga dhidi ya Syria, yatumia kombora jipya
Dec 16, 2024 08:01Utawala wa Kizayuni wa Israel unaendeleza mashambulizi yake makali dhidi ya maeneo mbalimbali ya Syria huku wanamgambo wanaoungwa mkono na nchi za Magharibi wakiwa wameipindua serikali ya nchi hiyo.
-
Wakurdi wa Syria wana wasiwasi wa kutokea Syria yaliyotokea Libya
Dec 16, 2024 08:00Msemaji wa kundi la SDF ambalo ni la Wakurdi wa Syria wanaoungwa mkono na Marekani amesema kuwa, wana wasiwasi wa kugeuka Syria kuwa Libya ya pili baada ya kuangushwa utawala wa Bashar al Assad.
-
Netanyahu aburuzwa tena mahakamani leo Jumatatu
Dec 16, 2024 07:51Duru mbalimbali za habari zikiwemo za Kizayuni zimeripoti kwamba, waziri mkuu wa Israel ambaye ni maarufu kwa jina la nduli wa Ghaza, ameburuzwa tena mahakamani leo Jumatatu kujibu shutuma za ufisadi na jinai zinazomuandamana yeye na familia yake.
-
Hamas: Taasisi za kimataifa zisaidie kufikisha misaada ya kitiba Ukanda wa Gaza
Dec 16, 2024 03:46Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imeziomba taasisi za kimataifa zitume misaada ya kitiba na kitabibu kwa ajili ya wakazi wa Ukanda wa Gaza.
-
Yemen: Marekani inatushambulia kwa sababu ya uungaji mkono wetu kwa wananchi wa Ghaza
Dec 15, 2024 23:12Mkuu wa Kamati ya Taifa ya Masuala ya Mateka wa serikali ya Yemen amesema kuwa, mashambulizi na tuhuma zinazotolewa na Marekani dhidi ya San'an kuhusu haki za binadamu ni muendelezo wa chuki za mabeberu dhidi ya Yemen kutokana na uungaji mkono wake usiotetereka wa wananchi wa Palestina hasa wa Ghaza.
-
Israel yashambulia magari 40 ya wagonjwa Ukanda wa Ghaza
Dec 15, 2024 23:10Taasisi ya Ulinzi wa Raia ya Ghaza imetangaza kuwa jeshi la Israel limeshambulia na kuharibu magari 40 ya kubebea wagonjwa katika ukanda huo tangu utawala wa Kizayuni ulipoanzisha mashambulizi yake ya kikatili yanayoendelea hadi hivi sasa dhidi ya Wapalestina.