-
Hizbullah: Makubaliano ya kusitisha vita Ghaza sharti la kusimama mashambulizi ya muqawama dhidi ya Israel
Mar 06, 2024 23:01Sheikh Naim Qassim, kiongozi wa ngazi ya juu wa harakati ya muqawama ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, kusitishwa mashambulizi ya Israel dhidi ya Ukanda wa Ghaza haraka iwezekanavyo kutaharakisha kusimamisha mapigano baina ya kusini wa Lebanon na maeneo Palestina yanayokaliwa kwa mabavu na Wazayuni tangu mwaka 1948 ambayo yamepachikwa jina bandia la Israel.
-
Muqawama wa Iraq waendeleza mashambulizi dhidi ya maeneo ya Wazayuni + VIDEO
Mar 06, 2024 23:00Makundi ya muqawama wa Kiislamu ya Iraq yametangaza kuwa yameendelea kuyashambulia maeneo mbalimbali ya utawala wa Kizayuni kwa kutumia droni (ndege zisizo na rubani) na kwamba mashambulizi hayo yataendelea hadi Israel itakapokomesha mashambulio yake dhidi ya Ukanda wa Ghaza.
-
Matokeo ya miezi 5 ya vita dhidi ya Gaza
Mar 06, 2024 22:59Miezi 5 ya vita dhidi ya Ukanda wa Gaza ambavyo vilikuwa havijawahi kushuhudiwa tena imekuwa na matokeo mbalimbali katika ngazi ya ndani, kikanda na kimataifa.
-
Hizbullah yayatwanga tena maeneo ya Wazayuni kwa mvua ya makombora
Mar 06, 2024 10:31Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imetangaza kuwa, imekitwanga kwa makumi ya makombora ya Katyusha, kitongoji cha walowezi wa Kizayuni cha Kfar Blum cha kaskazini mwa ardhi za Palestina zilizopachikwa jina bandia la Israel.
-
OIC yataka kukomeshwa jinai, uvamizi wa Israel dhidi ya Gaza
Mar 06, 2024 08:15Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imetoa mwito kusitishwa mara moja uvamizi na hujuma za kijeshi za utawala haramu wa Israel dhidi ya eneo la Ukanda wa Gaza.
-
Ukosoaji wa UN wa mashambulizi ya makusudi ya Israel dhidi ya misafara ya misaada huko Gaza
Mar 06, 2024 08:01Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki ya Chakula ametangaza kwamba, jeshi la Israel linashambulia kwa makusudi misafara ya misaada ya kibinadamu huko Gaza licha ya kujua njia za misafara hiyo.
-
Jeshi la Yemen lashambulia meli mbili za kivita za Marekani
Mar 06, 2024 04:00Msemaji wa jeshi la taifa la Yemen ameeleza kuwa jeshi hilo limezishambulia meli mbili za kivita za Marekani katika Bahari Nyekundu.
-
HAMAS yaitoa maanani ripoti ya UN ya madai ya 'ukatili wa kingono' katika Operesheni ya Oktoba 7
Mar 06, 2024 00:08Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imekanusha madai yaliyomo kwenye ripoti ya Umoja wa Mataifa inayodai kwamba wapiganaji wa harakati hiyo ya muqawama wa Palestina walifanya "ukatili wa kingono" wakati wa operesheni ya mashambulio waliyotekeleza dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel mnamo Oktoba 7, 2023.
-
Wataalamu: Baada ya siku 150, Israel haijafikia hata lengo moja la kijeshi katika vita vya Ghaza
Mar 06, 2024 00:07Wataalamu wa masuala ya kijeshi wamesema, baada ya kupita siku 150, utawala wa Kizayuni wa Israel haujaweza kufikia malengo uliyotangaza kuwa sababu ya kuanzisha vita dhidi ya Ukanda wa Ghaza, licha ya kuua maelfu ya Wapalestina, kujeruhi maelfu ya wengine, mbali na mamia ya maelfu walioachwa bila makazi pamoja na kuugeuza ukanda huo kuwa eneo la magofu.
-
Ulimwengu wa Kiislamu watakiwa ujiweke tayari kupambana vikali kwa ajili ya Palestina
Mar 06, 2024 00:06Spika wa Bunge la Uturuki Numan Kurtulmus ametoa wito kwa Ulimwengu wa Kiislamu kusimama na Palestina katika mapambano yake dhidi ya kukaliwa ardhi zake kwa mabavu na mauaji ya kimbari.