Hizbullah yayatwanga tena maeneo ya Wazayuni kwa mvua ya makombora
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i109204-hizbullah_yayatwanga_tena_maeneo_ya_wazayuni_kwa_mvua_ya_makombora
Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imetangaza kuwa, imekitwanga kwa makumi ya makombora ya Katyusha, kitongoji cha walowezi wa Kizayuni cha Kfar Blum cha kaskazini mwa ardhi za Palestina zilizopachikwa jina bandia la Israel.
(last modified 2024-03-06T10:31:37+00:00 )
Mar 06, 2024 10:31 UTC
  • Hizbullah yayatwanga tena maeneo ya Wazayuni kwa mvua ya makombora

Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imetangaza kuwa, imekitwanga kwa makumi ya makombora ya Katyusha, kitongoji cha walowezi wa Kizayuni cha Kfar Blum cha kaskazini mwa ardhi za Palestina zilizopachikwa jina bandia la Israel.

Shirika la habari la IRIB limeripoti habari hiyo leo Jumatano na kuongeza kuwa, shambulio hilo kubwa la makombora ya Hizbullah dhidi ya kitongoji cha walowezi wa Kizayuni cha Kfar Blum limepelekea kupigwa ving'ara vya hatari katika vitongoji vingine vya walowezi wa Kizayuni vya kaskazini mwa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni na limesababisha hasara kwenye kitongoji cha Wazayuni cha Kfar Blum. 

Baada ya shambulio hilo kubwa la Hizbullah dhidi ya Wazayuni, vyombo vya habari vya Israel vimeripoti kuwa, umeme umekatika kwenye maeneo mengi ya mji wa al Jalil Kaskazini. 

Harakati ya Hizbullah imetangaza kuwa shambulio hilo ni majibu ya shambulizi lililofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya kitongoji cha Jula cha Lebanon ambalo liliua shahidi watu watatu wa familia moja na kujeruhi wengine kadhaa.

Mashambulio ya Hizbullah ya Lebanon yamekuwa yakiwasababishia hasara kubwa Wazayuni

 

Taarifa zinasema kuwa, katika shambulio lake la kulipoiza kisasi, Hizbullah ilianza kurusha makombora ya kuuchanganya na kuubabaisha mfumo wa kujilinda na makombora wa Israel na ndipo Hizbullah ikatumia fursa hiyo kukitwanga kwa makumi ya makombora kitongoji cha walowezi wa Kizayuni cha Kfar Blum. 

Mwishoni mwa mwezi uliopita wa Februari pia, Hizbullah ya Lebabanon ililitwanga kwa makombora kundi la wanajeshi vamizi wa Israel katika kambi kadhaa tofauti za kijeshi za utawala wa Kizayuni.

Harakati hiyo ya Hizbullah ya Lebanon ilisema katika taarifa yake kwamba imezipiga kwa makombora kambi nne za kijeshi za Israel ikiwemo ile ya Zabdin wakati wanajeshi wa utawala wa Kizayuni walipokuwa wamekusanyika huko.