Jeshi la Yemen lashambulia meli mbili za kivita za Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i109182-jeshi_la_yemen_lashambulia_meli_mbili_za_kivita_za_marekani
Msemaji wa jeshi la taifa la Yemen ameeleza kuwa jeshi hilo limezishambulia meli mbili za kivita za Marekani katika Bahari Nyekundu.
(last modified 2024-03-06T04:00:52+00:00 )
Mar 06, 2024 04:00 UTC
  • Jeshi la Yemen lashambulia meli mbili za kivita za Marekani

Msemaji wa jeshi la taifa la Yemen ameeleza kuwa jeshi hilo limezishambulia meli mbili za kivita za Marekani katika Bahari Nyekundu.

Brigedia Jenerali Yahya Saree ameeleza kuwa jeshi shupavu la Yemen limezishambulia meli mbili za kivita za Marekani katika Bahari Nyekundu katika kuwaunga mkono wananchi madhulumu wa Palestina na kujibu uvamizi wa Marekani na Uingereza dhidi ya Yemen. 

Brigedia Jenerali Saree amesema kuwa jeshi la taifa la Yemen limetumia makombora ya baharini na droni katika oparesheni hiyo dhidi ya Marekani. Msemaji wa jeshi la taifa la Yemen amesisitiza kwa mara nyingine tena kwamba wataendelea kutekeleza oparesheni zao hadi pale vita vitakapositishwa Ukanda wa Gaza na mzingiro kuondolewa katika eneo hilo.  

Vikosi vya jeshi la Yemen vimeeleza kuwa vitaendeleza kuzishambulia katika Bahari Nyekundu meli zote za utawala wa Kizayuni au zile zinazoelekea katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) hadi hapo utawala wa Kizayuni utakaposimamisha mashambulizi yake ya kikatili dhidi ya Gaza.  

Ansarullah ya Yemen na oparesheni dhidi ya meli za wavamizi 

Huku haya yakiripotiwa, muqawama wa Kiislamu wa Iraq leo asubuhi umetangaza kuwa umekishambulia kiwanda cha kuzalisha umeme katika uwanja wa ndege wa mji wa Haifa huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Kiwanda hicho cha kuzalisha umeme kimeshambuliwa kwa droni.