-
Jeshi la Yemen latekeleza operesheni nyingine dhidi ya meli ya Marekani katika Bahari Nyekundu
Feb 12, 2024 06:51Msemaji wa jeshi la Yemen ametangaza kuwa vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo vimetekeleza operesheni nyingine dhidi ya meli ya Marekani katika Bahari Nyekundu.
-
Mauaji ya kimbari ya Israel dhidi ya Gaza: Raia 100 wauawa Rafah, mamia wajeruhiwa
Feb 12, 2024 04:31Utawala katili wa Israel umeendeleza mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza kwa kutekeleza mashambulizi makubwa ya anga na mizinga katika mji wa Rafah kusini mwa ukanda huo na kuua na kujeruhi mamia ya raia, wengi wao wakiwa wanawake na watoto.
-
Zaidi ya wanajeshi 11 wa Israel wauawa katika "shambulio kubwa" huko Khan Yunis
Feb 12, 2024 01:09Vyombo vya habari vya Israel vimeripoti kwamba, jeshi la utawala huo ghasibu limekabiliwa na shambulio kubwa na la kushtukiza la wapiganaji wa Wapalestina huko Khan Yunis, kusini mwa Ukanda wa Gaza, ambalo limeua zaidi ya wanajeshi 11 wa utawala huo.
-
Hizbullah yaonya dhidi ya sera ya kupenda vita ya Israel
Feb 12, 2024 01:07Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema mrengo wa muqawama haujatangaza vita kamili, lakini iwapo Israel itapanua vita vyake vya Gaza, wanamuqawama hawatasita kufanya mashambulizi ya kujibu chokochoko za adui huyo mpenda vita.
-
Kukiri Netanyahu kuweko mgogoro mkubwa wa kiuchumi Israel
Feb 11, 2024 22:48Benjamin Netanyahu, waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni amekiri kwamba utawala dhalimu wa Israel umekumbwa na mgogoro mkubwa wa kiuchumi hivi sasa.
-
Wanajeshi saba wa Israel waangamizwa na muqawama Khan Yunis
Feb 11, 2024 00:33Wanajeshi saba wa utawala vamizi wa Israel wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mji wa Khan Yunis huko Palestina.
-
Kukiri UN juu ya nafasi chanya ya Iran katika matukio ya Asia Magharibi
Feb 11, 2024 00:31Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameeleza wasiwasi wake kuhusu kuenea hali ya mivutano katika eneo la Magharibi mwa Asia na kusema Iran ina nafasi chanya na yenye taathira katika matukio ya eneo hilo na katika kurejesha amani na utulivu.
-
Msemaji wa Maulamaa wa Palestina: Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yamebadilisha historia ya dunia
Feb 10, 2024 07:10Mkuu wa Baraza la Ushauri na Msemaji wa Baraza Kuu la Maulamaa wa Palestina amesema kuwa, Mapinduzi ya Kiislamu ya nchini Iran si kwa ajili ya nchi hiyo tu bali ni kwa ajili ya ulimwengu mzima kwani yamebadilisha sura ya historia ya dunia.
-
Mwanajeshi wa Israel aliyefanya uhalifu huko Gaza atangaza toba na kusilimu
Feb 10, 2024 03:53Mwanajeshi wa Israel ametamka Shahada Mbili na kutangaza kusilimu, akisisitiza kuwa amepata usalama wa kinafsi na toba katika dini ya Uislamu baada ya picha za ukatili alioufanya yeye na wenzake katika jeshi la Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, kumuandamana wakati wote.
-
Haaretz: Uharibifu wa Gaza unafanana na "hali ya baada ya bomu la atomiki"
Feb 10, 2024 03:52Gazeti la Israel la Haaretz limetumia picha za angani za kabla na baada ya vita vinavyoendelea kwenye Ukanda wa Gaza, kuashiria ukubwa wa uharibifu uliosababishwa na jeshi la Israel, likieleza hali hiyo ya uharibifu mkubwa kuwa ni sawa na ile ya baada ya bomu la atomiki.