Wanajeshi saba wa Israel waangamizwa na muqawama Khan Yunis
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i108234-wanajeshi_saba_wa_israel_waangamizwa_na_muqawama_khan_yunis
Wanajeshi saba wa utawala vamizi wa Israel wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mji wa Khan Yunis huko Palestina.
(last modified 2024-02-11T00:33:01+00:00 )
Feb 11, 2024 00:33 UTC
  • Wanajeshi saba wa Israel waangamizwa na muqawama Khan Yunis

Wanajeshi saba wa utawala vamizi wa Israel wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mji wa Khan Yunis huko Palestina.

Mujahidina wa Brigedi za Izzuddin Qassam tawi la Kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS wamekabiliana na wanajeshi wa Israel mashariki mwa Khan Yunis kusini mwa Ukanda wa Gaza na kuwaangamiza watano kati yao.

Wanajeshi hao wa Iisrael waliangamizwa baada ya kuripukiwa na bomo katika eneo moja mashariki mwa Khan Yunis.

Kuuawa kwa wanajeshi hao saba wa jeshi la utawala haramu wa Israel huko Khan Yunis kunaifanya idadi ya askari Israel walioangamizwa hadi sasa tangu ilipototekelezwa operesheni ya Kimbunga cha al-Aqswa kukaribia 600.

 

Baadhi ya ripoti zinasema kuwa, idadi ya askari wa Israel waliouawa ni zaidi ya hiyo hasa kutokana na mamlaka husika kutotoa takwimu sahihi.

Utawala dhalimu wa Israel ambao umeshindwa kwenye medani za mapambano, umeamua kumalizia hamaki zake kwa kuua watoto wadogo, wanawake, vizee na raia wa kawaida huko Gaza.

Katika upande mwingine, imeelezwa kuwa, wakati mfumo wa afya ya akili wa Israel unakabiliwa na hatari ya kuporomoka, madaktari wa magonjwa ya akili wanaondoka kuelekea Uingereza kutafuta hali bora zaidi ya maisha.

Kugura huko kwa madaktari wa afya ya akili kunakuja wakati mahitaji ya huduma za afya ya akili huko Israel yanaongezeka kutokana na vita vya Gaza, na kwamba wiki iliyopita wakuu wa vituo vya afya ya akili walituma barua kwa Mdhibiti wa Serikali, Matanyahu Englman, wakionya kwamba "mfumo wa afya ya akili wa Israel unakaribia kusambaratika kabisa.”