Mwanajeshi wa Israel aliyefanya uhalifu huko Gaza atangaza toba na kusilimu
Mwanajeshi wa Israel ametamka Shahada Mbili na kutangaza kusilimu, akisisitiza kuwa amepata usalama wa kinafsi na toba katika dini ya Uislamu baada ya picha za ukatili alioufanya yeye na wenzake katika jeshi la Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, kumuandamana wakati wote.
Taarifa ya televisheni ya Al Jazeera imeripoti kuwa, kupitia matangazo ya moja kwa moja na mwanaharakati Muislamu kwenye mitandao ya kijamii, mwanajeshi huyo wa Israel - ambaye jina lake halikutajwa, - amefichua kusilimu kwake, baada ya kuandamwa na picha za wahanga wake na kukosa usingizi.
Kuhusu sababu ya kusilimu kwake, mwanajeshi huyo wa Israel amesema, “Kwa kweli, Uislamu ulinivutia, kwa sababu katika kitabu kitakatifu cha Mayahudi tunafundishwa kuua watoto, wanawake, wanyama na kila kitu.”
Mwanajeshi huyo wa Israel amezungumza kuhusu ukatili aliofanya na wenzake dhidi ya Wapalestina wasio na ulinzi, wakiwemo watoto, katika Ukanda wa Gaza, na kufichua mbinu za mauaji na mateso wanayofanya tena kwa furaha kubwa.
Miongoni mwa njia hizo ni kujaribu kuua watoto kwa kuwafungulia mbwa wakali. Askari huyo wa Israel anakiri akisema, "Tulikuwa tukifanya mambo ya kutisha. Kwa mfano, tulikuwa tukirusha mabomu ya kushtua ndani ya nyumba Wapalestina na kuchekelea ..."
Amesimulia kwamba wakati mmoja walimfungulia mtoto wa Kipalestina mbwa aliyekuwa akibweka, na kwamba mtoto huyo alianza kujikojolea kwa hofu kubwa.
Mwanajeshi huyo wa Kiisraeli pia amesema kwamba wanawafundisha watoto wao tangu utotoni kwamba Waarabu watakuwa watumwa wa Wayahudi.