-
Picha za satelaiti zaonyesha Israel ikijimarisha kuwepo kijeshi katika Ukanda Gaza
Dec 21, 2025 04:26Utawala wa Israel unaonekana kuandaa mazingira ya kudumisha uwepo wake kijeshi katika maeneo makubwa ya Ukanda wa Gaza. Hii ni kwa mujibu wa uchambuzi mpya wa picha za satelaiti ulioweka wazi ujenzi mkubwa, upanuzi wa miundombinu na kuendelea kuharibiwa mali za Wapalestina tangu kutekelezwa mapatano ya usitishaji vita mwezi Oktoba.
-
Ripoti: Watoto wa Gaza wanateseka na baridi kali
Dec 20, 2025 23:05Dhoruba za majira ya baridi kali zimesababisha vifo vya Wapalestina wasiopungua 17 katika Ukanda wa Gaza mwezi huu wa Disemba pekee.
-
Hamas yalaani shambulizi la kikatili dhidi ya shule katika mji wa Gaza
Dec 20, 2025 09:24Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imelaani shamulizi la kikatili la Israel dhidi ya shule moja katika mji wa Gaza lililouwa Wapalestina kadhaa. Hamas imeitaja hujuma hiyo kuwa jinai ya kivita ya makusudi na ukiukaji wa wazi wa mapatano ya kusitisha mapigano.
-
Katibu Mkuu wa UN akemea kuongezeka kwa ukatili wa walowezi wa Kizayuni Ukingo wa Magharibi
Dec 20, 2025 03:36Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amelaani kuongezeka kwa mashambulizi ya walowezi wa Kizayuni wasiokuwa halali dhidi ya raia wa Kipalestina wasio na silaha na mali zao katika maeneo ya Ukingo wa Magharibi yanayokaliwa kwa mabavu na Israel.
-
Wayemen waandamana kupinga kuvunjiwa heshima Qur'an Marekani
Dec 19, 2025 23:08Makumi ya maelfu ya wananchi wa Yemen walimiminika katika barabara na mitaa ya Sa’ada jana Ijumaa kushiriki maandamano ya kulaani kitendo cha kunajisiwa Qur'ani Tukufu nchini Marekani, sanjari na kupaza sauti zao kuiunga mkono Palestina, huku hasira zikiongezeka katika ulimwengu wa Kiislamu kutokana na wimbi la vitendo vya hivi karibuni vilivyo dhidi ya Uislamu na Waislamu.
-
UAE, mnunuzi wa siri katika mkataba mkubwa wa silaha na Israel
Dec 19, 2025 23:04Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) umetambuliwa kama mnunuzi 'asiyejulikana' kwenye mkataba wa dola bilioni 2.3 uliosainiwa mwezi uliopita na kampuni za kuzalisha silaha ya Israel ya Elbit Systems, ripoti inasema.
-
Katika kuitajirisha sekta ya silaha ya US, Qatar nayo yaomba kuuziwa ndege za F-35
Dec 18, 2025 23:55Vyombo vya habari vya Israel vimetangaza kuwa, Qatar imefanya mazungumzo na Marekani kuhusu kununua nchi hiyo ya Kiarabu ndege za kisasa za kivita za Marekani aina ya F-35.
-
Netanyahu atangaza kuidhinisha mauzo ya 'kihistoria' ya gesi ya dola bilioni 35 kwa Misri
Dec 18, 2025 23:54Waziri mkuu wa utawala wa kizayuni wa Israel, Benjamin Netanyahu ametangaza kuwa, serikali yake imeidhinisha makubaliano makubwa ya uuzaji wa gesi asilia kwa Misri yenye thamani ya karibu dola bilioni 35, akielezea kwamba makubaliano hayo ni makubwa zaidi katika historia ya Israel kwa upande wa thamani na ujazo wa usafirishaji nje.
-
Itifaki ya kimataifa kuhusu haki ya Wapalestina ya kujiainishia hatima yao
Dec 18, 2025 22:48Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) limeunga mkono haki ya Wapalestina ya kujiainishia hatima na mustakabali wao.
-
Kwa nini Uturuki haiko tayari kubadilisha misimamo yake kuhusu Gaza?
Dec 18, 2025 10:02Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki ametangaza kwamba nchi yake haitarudi nyuma na wala haitaachana na misimamo yake kuhusu Gaza.