-
Mbali na kuua watoto wachanga, Wazayuni wanafanya uporaji pia Ghaza
Dec 23, 2023 23:09Mkuu wa Ofisi ya Upashaji Habari ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa mbali na jinai zao nyingine nyingine kama za kuua watoto wachanga, wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wanafanya uporaji pia wa mali za Wapalestina wakati wanapoingia kwenye nyumba walizozivunja kwa mashambulizi ya kikatili na kinyama huko Ghaza.
-
Wanajeshi wa Israel walioangamizwa na wanamuqawa wakaribia 500
Dec 23, 2023 08:40Idadi ya wanajeshi wa utawala haramu wa Israel walioangamizwa na wanamuqawama wa Palestina inazidi kuongezeka sambamba na wanajeshi wa jeshi hilo kuingiwa na kiwewe kutokana na operesheni za kijeshi dhidi yao katika Ukanda wa Gaza.
-
Wanasiasa wataka kufunguliwa mashitaka Wafaransa waliojiunga na jeshi la Israel kuua raia Gaza
Dec 23, 2023 08:29Katika kashfa mpya ambayo inaendelea kutikisa misingi ya jamii ya Ufaransa na sambamba misimamo ya inayobadilika badilika ya serikali ya Paris kuhusu mashambulizi ya Israel Ukanda wa Gaza, mbunge Thomas Portes wa chama cha "Fahari ya Ufaransa" amefichua uwepo wa Wafaransa 4,185 katika safu za jeshi la Israel linaloendelea kuua raia wa Palestina hususan wanawake na watoto wa Gaza.
-
Uchunguzi wa maoni: Asilimia 96 ya Wasaudia wanapinga nchi yao kuanzisha uhusiano na Israel
Dec 23, 2023 07:48Uchunguzi wa maoni unaonyesha kuwa, wananchi wengi wa Saudi Arabia wanapinga nchi yao kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.
-
Umoja wa Mataifa wataka misaada zaidi Gaza baada ya kupasiswa azimio
Dec 23, 2023 07:48Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa mwito wa kuongezwa misaada zaidi ya kibinadamu kwa watu wa Gaza wanaokabiliwa na hali mbaya ya uhaba wa chakula na huduma zingine muhimu.
-
Azimio la Baraza la Usalama kuhusu Gaza: Ni hatua ya lazima lakini haitoshi
Dec 23, 2023 04:48Ijumaa ya jana, Desemba 22, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio la kuongeza misaada ya kibinadamu kwa watu wa Ukanda wa Gaza bila kutoa wito wa kusitishwa mapigano. Marekani na Russia, wanachama wawili wa kudumu wa Baraza la Usalama, hazikulipigia kura azimio hilo. Wajumbe wengine 13 wamelipigia kura ya ndiyo.
-
Wanajeshi wa Israel washambulia waumini wa Kiislamu karibu na Msikiti wa Al-Aqsa
Dec 23, 2023 03:26Mji wa Al-Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel Ijumaa ulishuhudia vikosi vya Israel vikitumia gesi ya kutoa machozi na nguvu ziada kwa ajili ya kuwatawanya waumini karibu na eneo la Msikiti wa Al-Aqsa huku watu wengi wakiugua kwa kuvuta gesi hiyo ya machozi.
-
HAMAS: Azimio la Baraza la Usalama la UN kuhusu Gaza halitoshi kukidhi mahitaji
Dec 22, 2023 23:18Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imetoa mjibizo kwa azimio lililopitishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Ukanda wa Gaza na kusisitiza kuwa halitoshi na halikidhi mahitaji.
-
Al-Wefaq: Bahrain imewasaliti Wapalestina kwa kujiunga na muungano wa US
Dec 22, 2023 22:57Chama kikuu cha upinzani nchini Bahrain cha al-Wefaq kimesema hatua ya utawala wa Aal-Khalifa ya kujiunga na muungano wa baharini wa Marekani katika Bahari Nyekundu ni kusaliti kadhia ya Palestina.
-
Muungano wa baharini dhidi ya Yemen wapata kipigo kingine; Kampuni zingine mbili zaacha kupita Bahari Nyekundu
Dec 22, 2023 07:17Muungano mpya wa baharini unaoongozwa na Marekani umepata kipigo kipya baadea ya makampuni mawili ya Hapag-Lloyd la Ujerumani na OOCL la Hong Kong kutangaza kuwa yatasimamisha safari za meli zao kupitia Bahari Nyekundu hadi ilani nyingine itakapotolewa.