Wanajeshi wa Israel walioangamizwa na wanamuqawa wakaribia 500
Idadi ya wanajeshi wa utawala haramu wa Israel walioangamizwa na wanamuqawama wa Palestina inazidi kuongezeka sambamba na wanajeshi wa jeshi hilo kuingiwa na kiwewe kutokana na operesheni za kijeshi dhidi yao katika Ukanda wa Gaza.
Duru za kijeshi za Israel zimetangaza kuwa, idadi ya wanajeshi wake waliouawa huko Gaza imefikia 472 baada ya wanajeshi wake kadhaa kuuawa jana na leo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wanajeshi 140 wa Kizayuni wameangamizwa tangu jeshi la Israel lilipoanzisha operersheni ya kijeshi ya nchi kavu huko Gaza.
Baadhi ya vyombo vya habari vikizinukuu duru za karibu na jeshi la Israel zinasema kuwa, miongoni mwa wanajeshi wa Israel waliouawa hadi sasa wapo makamanda na majerali muhimu wa Israel.
Hayo yanajiri siku moja tu baada ya Brigedi za Izzuddin Al Qassam tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) kupigana na kundi moja la makomando wa utawala wa Kizayuni katika eneo la al Toam kaskazini mwa mji wa Gaza hapo jana; ambapo wanajeshi 11 wa kikosi maalumu cha Israel wameangamizwa.
Brigedi za Izzuddin al Qassam zilitangaza kwamba zimeendelea kuipiga kwa makombora miji ya utawala wa Kizayuni ukiwemo mji mkuu Tel Aviv ili kujibu jinai za Israel dhidi ya Wapalestina wa Gaza.
Utawala dhalimu wa Israel ambao umeshindwa kwenye medani za mapambano, umeamua kumalizia hamaki zake kwa kuua watoto wadogo, wanawake, vizee na raia wa kawaida huko Gaza.
Wakati huo huo, harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imesema wazi kwamba hakuna mabadilishano yoyote ya mateka yatakayofanyika ila baada ya utawala wa Kizayuni kukomesha kikamilifu jinai zake dhidi ya wananchi wa Gaza.