-
Tamasha la Asubuhi: Sauti ya Muqawama dhidi ya ubeberu wa kimataifa, linaendelea Tehran
May 07, 2025 06:37Tamasha la tatu la vyombo vya habari la "Sobh", (Asubuhi) kwa ajili ya kuwaenzi watu mashuhuri wanaopinga ubeberu, kuanzia wabunge wa zamani wa mabunge ya Ulaya na Uingereza hadi mwandishi wa habari wa Palestina kutoka Gaza, linaendelea kupaza sauti ya mapambano na Muqawama dhidi ya ukandamizaji wa kimataifa.
-
Abu Ubaidah: Wapalestina hawatosahau Wayemen walivyosimama nao bega kwa bega
Apr 14, 2025 06:11Msemaji wa Brigedi za Izzuddinul-Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema, Wapalestina hawatosahau namna Wayemen walivyosimama imara na bega kwa bega pamoja nao katika Jihadi ya kuikomboa ardhi ya Palestina.
-
Wanazuoni wa Kiislamu watoa fatwa; Mataifa ya Kiislamu yaunge mkono Muqawama wa Palestina
Apr 05, 2025 07:19Umoja wa Kimataifa wa Wanazuoni wa Kiislamu (IUMS) umetoa fatwa (agizo la kidini) ukizitaka nchi za Kiislamu kutoa msaada wa haraka wa kijeshi, kifedha na silaha kwa mrengo wa Muqawama wa Palestina, ili kukabiliana na mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na utawala katili wa Israel katika Ukanda wa Gaza.
-
Iran, Lebanon, Iraq, Yemen zaanza luteka ya kuwaunga mkono Wapalestina Gaza
Mar 27, 2025 11:30Vikosi vya Baharini vya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) pamoja na vikosi kutoka Lebanon, Iraq na Yemen, vinafanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi ya majini katika 'maonyesho ya nguvu' dhidi ya Israel na kutangaza mshikamano na Wapalestina huko Gaza.
-
"Mantiki ya Muqawama ya IRGC ndiyo njia pekee ya kuwaokoa Waislamu"
Mar 11, 2025 04:39Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) Meja Jenerali Hossein Salami amesema mantiki ya Muqawama ya SEPAH ndiyo njia pekee ya kuwaokoa Waislamu mkabala wa kutawaliwa na maadui.
-
Spika Qalibaf: Namna Hizbullah ilivyoonyesha nguvu zake imedhihirika kuwa Muqawama hauondosheki
Feb 25, 2025 10:39Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amesema, kutokana na jinsi Hizbullah ilivyoonyesha nguvu na uwezo wake, imemdhihirikia wazi kila mtu kwamba maadui hawawezi kuuondoa Muqawama au kuuweka kando ya ulingo wa kisiasa na kiusalama wa Lebanon kutokana na uungaji mkono wa wananchi ilionao.
-
HAMAS: Kuwa na silaha ni haki ya kisheria ya Muqawama na kuachana nazo ni jambo lisilowezekana
Feb 25, 2025 09:46Hazem Qassem, msemaji wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS ameashiria matamshi yaliyonasibishwa na kiongozi mwandamizi wa harakati hiyo Musa Abu Marzouk na kusisitiza kwamba: "Hamas inaendelea kutumia silaha za Muqawama kama haki halali na ya kisheria na haitalegeza msimamo juu ya suala hilo".
-
Iran kuwakilishwa na Spika wa Bunge, Waziri wa Mambo ya Nje katika mazishi ya Shahidi Nasrallah
Feb 23, 2025 03:47Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) Mohammad Baqer Qalibaf na Waziri wa Mambo ya Nje Abbas Araghchi leo wanaelekea Beirut kushiriki katika hafla ya mazishi ya kiongozi wa Hizbullah aliyeuawa shahidi, Sayyed Hassan Nasrallah, pamoja na mkuu wa Baraza la Utendaji la Hizbullah, Shahidi Sayyid Hashim Safieddine.
-
Salami: Njama za US, Israel kudhuru Muqawama zimegonga mwamba
Feb 21, 2025 07:36Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC), Meja Jenerali Hossein Salami amesema, hakuna shaka kwamba juhudi za Marekani na utawala wa Kizayuni za kujaribu kuudhuru mrengo wa Muqawama zitafeli na kugonga mwamba.
-
Iran: Tunapinga mpango wowote wa kufukuzwa Wapalestina Gaza
Feb 19, 2025 12:07Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran), Mohammad Bagher Ghalibaf amesema kuwa Tehran inapinga vikali na kulaani mpango wowote unaokusudia kuwafurusha Wapalestina katika ardhi zao.