-
Lieberman: Makombora ya Iran yamebadilisha kanuni za vita na hatujajiandaa kukabiliana nayo
Jan 20, 2026 00:45Kiongozi wa chama cha Yisrael Beiteinu, Avigdor Lieberman, ameonya kuhusu tishio linaloongezeka la Iran, akidai kwamba, makombora ya Iran yamebadilisha kanuni za vita na kutoa wito wa maandalizi ya kuhamisha vituo nyeti vya kimkakati kwa kutarajia mzozo wowote tarajiwa.
-
Palestina: Idadi ya watoto wanaozaliwa wakiwa vilema inaongezeka
Jan 19, 2026 22:41Mkuu wa idara ya habari ya Wizara ya Afya ya Palestina huko Gaza ametangaza kuwa, idadi ya watoto wanaozaliwa wakiwa vilema inazidi kuongezeka katika Ukanda huo unaokabiliwa na hali mbaya ya kibinadamu.
-
Makanisa ya al-Quds yaonya kuwa ‘Uzayuni wa Kikristo’ unahatarisha Ukristo
Jan 19, 2026 03:50Viongozi wakuu wa Kikristo katika mji wa Palestina wa al-Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na Israel, wameonya kuwa “Uzayuni wa Kikristo” pamoja na ajenda za nje zinavunja umoja wa Wakristo katika Ardhi Takatifu na kudhoofisha mamlaka yao ya kiroho na kijamii.
-
Waziri Mkuu wa Iraq akosoa mauaji Ghaza na Lebanon na vitisho dhidi ya Iran
Jan 18, 2026 03:33Waziri Mkuu wa Iraq amekosoa vikali unyama na mauaji ya kigaidi huko Ghaza na Lebanon, mashambulizi yanayoendelea kufanywa na Israel nchini Syria, pamoja na tishio dhidi ya Iran ambayo ni nchi jirani na Iraq.
-
Amr Moussa atoa indhari kali kwa Saudia na Misri kuhusiana na utawala wa kizayuni wa Israel
Jan 17, 2026 23:41Katibu Mkuu wa zamani wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu ametoa indhari kali kwa Saudi Arabia na Misri kuhusiana na hatua zinazochukuliwa na utawala wa kizayuni wa Israel na akasema: kinachojiri hivi sasa si suala dogo na la pembeni bali ni "tishio la kimkakati" kwa usalama wa nchi za Kiarabu na eneo kwa ujumla.
-
Marekani yatangaza wajumbe wa iitwayo 'Bodi ya Amani' ya Ghaza, yumo pia Tony Blair
Jan 17, 2026 23:09Ikulu ya White House imetangaza majina ya wajumbe wa linaloitwa baraza la amani litakaloongozwa na Rais wa Marekani Donald Trump na kusimamia utawala wa eneo la Palestina la Ukanda wa Ghaza. Orodha hiyo inajumuisha waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mark Rubio, mjumbe maalumu wa Trump Steve Witkoff, mkwe wa Trump Jared Kushner, na waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair.
-
Mchambuzi Mzayuni: Marekani haina uthubutu wa kuanzisha vita vingine dhidi ya Iran
Jan 16, 2026 23:01Mchambuzi mmoja wa masuala ya kieneo na kimataifa wa utawala wa Kizayuni amesema kuwa, si Donald Trump na si Marekani yenyewe, wote hawana uthubutu wa kuanzisha vita vipya dhidi ya Iran.
-
Jumuiya ya Shanghai yalaani ghasia za kigaidi nchini Iran huku uungaji mkono kimataifa ukiongezeka
Jan 16, 2026 03:48Norlan Yerkembayev Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) amelaani vikali hujuma za kigaidi na uharibifu wa hivi karibuni katika mji wa Tehran na miji mingine ya Iran iliyoathiriwa wakati wa maandamano ya amani ya wananchi.
-
Kiongozi wa Ansarullah: Taifa la Iran limetibua njama ya adui kwa maandamano ya mamilioni ya wananchi
Jan 16, 2026 03:45Kiongozi wa harakati ya muqawama ya Ansarullah ya Yemen amesema kuwa Marekani na Israel ziliwaweka magaidi vibaraka wao ili kuchochea machafuko Iran kupitia kuchoma moto misikiti na kuuwa vikosi vya usalama na raia hata hivyo taifa la Iran limetoa jibu madhubuti kwa hujuma hiyo kwa maandamano makubwa ya mamilioni ya wananchi kote nchini kulaani ghasia na machafuko.
-
Kamati ya Wateknokrati wa kuendesha Ghaza kukutana kwa kikao cha kwanza mjini Cairo, Misri
Jan 15, 2026 06:58Mipango inaendelea kupangwa kuhakikisha wajumbe wa kamati ya wateknokrati iliyoteuliwa kuendesha masuala ya Ghaza kusafiri hadi Misri kwa mkutano wake wa kwanza, uliotarajiwa kufanyika leo Alkhamisi au kesho Ijumaa. Hayo ni kwa mujibu wa chanzo kimoja cha habari cha Palestina.