-
Netanyahu: Israel haitaondoka katika maeneo ya kusini ya Syria iliyoyavamia
Dec 08, 2025 03:00Waziri Mkuu wa utawala wa kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu amesema, jeshi la utawala huo halitaondoka katika maeneo liliyoyavamia na kuyakalia kwa mabavu ya kusini mwa Syria.
-
HAMAS: Tuko tayari kukabidhi silaha kwa utawala wa Wapalestina ikiwa Israel itaondoka kikamilifu Ghaza
Dec 07, 2025 23:04Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imesema, iko tayari kukabidhi silaha zake katika Ukanda wa Ghaza kwa mamlaka ya utawala ya Wapalestina itakayosimamia uendeshaji wa eneo hilo, kwa sharti kwamba uvamizi na ukaliaji ardhi kwa mabavu wa jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel ukomeshwe kikamilifu.
-
Qatar yakanusha kuisaidia kifedha HAMAS, yasema mawasiliano yao yalianza miaka 13 nyuma
Dec 07, 2025 23:03Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar amesema mawasiliano baina ya Doha na harakati ya Hamas yalianza miaka 10 hadi 13 iliyopita kwa lengo la kurahisisha juhudi za kusitisha mapigano na kupeleka misaada ya kibinadamu Ghaza.
-
Uhispania: Ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni ni kinyume na sheria za kimataifa
Dec 07, 2025 03:20Serikali ya Uhispania imetangaza kuwa, ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni unaofanywa na utawala wa Israel katika maeneo ya Wapalestina ni kinyume na sheria za kimataifa.
-
Amnesty International yaonya kuhusiana na hali ya Gaza
Dec 07, 2025 03:19Katibu Mkuu wa Amnesty International sambamba na kueleza wasi wasi wake mkubwa kuhusu hali ya Gaza amesisitiza kuwa: Jamii ya kimataifa imejitenga kuiwajibisha Israel na haiangazii na kuzingatia tena hali ya Gaza.
-
Kamari kubwa ya Israel Ghaza yashindwa vibaya kwa kuangamizwa Abu Shabab
Dec 06, 2025 22:55Kuangamizwa kiongozi wa genge la kigaidi na mamluki wa Israel katika Ukanda wa Ghaza, ni kufeli njama za kijasusi za utawala huo huko Ghaza na ni uthibitisho kwamba njama za kutafuta kundi la kuchukua nafasi ya Hamas ni kamari isiyo na mwisho.
-
Imarati yawalipa magaidi mamilioni ya dola kumuokoa mwanamfalme
Dec 06, 2025 22:53Muungano wa Falme za Kiarabu (Imarati) imewalipa magaidi wa al-Qaeda zaidi ya dola milioni 23 kama kikomboleo cha mwanamfalme aliyekuwa ametekwa nyara na magaidi hao huko Mali, magharibi mwa Afrika.
-
Mamluki wa Saudia na Imarati watwangana Hadhramaut Yemen
Dec 06, 2025 22:52Muungano wa Kikabila wa Hadramaut wa vibaraka wa Saudi Arabia umeanzisha mashambulio makali dhidi ya vibaraka wa Muungano wa Falme za Kiarabu (Imarati) ukitangaza kwamba kundi la Imarati limekanyaga makubaliano ya kusitisha vita baina yao na linahusika na mauaji yanayoendelea hivi sasa katika jimbo hilo.
-
Jumuiya ya Wafungwa wa Palestina: Israel ina mpango wa kumuua Marwan Barghouthi
Dec 06, 2025 10:12Kundi la kutetea wafungwa wa Kipalestina, The Palestinian Prisoners’ Society (PPS), limeonya juu ya njama hatari ndani ya magareza ya Israel ya kumuua kiongozi mtajika wa Palestina, Marwan Barghouthi, aliyetekwa nyara huku kukiwa na ripoti za ukandamizaji na kudhalilishwa pakubwa kiongozi huyo wa Palestina.
-
Katibu Mkuu wa Hizbullah: Lebanon inakabiliwa na uchokozi hatari wa Israel
Dec 06, 2025 09:42Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon Sheikh Naim Qassem amesema kuwa Lebanon inakabiliwa na uchokozi hatari na wa kujitanua wa Israel ambao unapasa kukabiliwa kwa njia zote.